Friday, May 31, 2013

Photos: Afariki baada ya kuanguka akidandia daladala, Dar

afariki-akidandia-daladala-0

afariki-akidandia-daladala
Mtu mmoja ambaye jina lake bado halijafahamika, amefariki dunia baada ya kuteleza na kuanguka wakati alipokua akijaribu kudandia Daladala maeneo ya Ilala Boma, Jijini Dar es Salaam, asubuhi leo. Marehemu huyo baada ya kuanguka na kupiga kichwa kwenye lami, alipasuka kichwa na kuvuja damu nyingi kichwani, na kufariki katika eneo la tukio.


Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Amana, Ilala. Kwa habari na picha zaidi, nenda kwenye link ifuatayo:
Source: bongoclantz

ANGALIA RAIA ZINAUZA UTU BIGBRAZA,.PESA BWANA

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA

Matokeo  ya  kidato cha sita nayo yapo hewani.....Ukitaka  kuyaangalia  bofya  link  zifuatazo


au

update za Kifo chake Ngwea By Millard Ayo

Kifo chake Ngwea
By Millard Ayo | Fri, 31 May 2013



Mpaka sasa bado unaendelea utaratibu wa kusafirisha mwili wa Marehemu Albert Mangwea kutoka Johannesburg, South Africa, kutoka kwenye mochwari ya serikali ya Hillbrow.

Mangwea alifariki dunia 28 May akiwa Johannesburg, alipokuja kufanya show ambazo Watanzania wa huku wanasema mara ya mwisho kuonekana kwenye stage ilikua wiki tatu zilizopita.

Bado chanzo cha kifo hakijajulikana na bado pia majibu ya uchunguzi wa Madaktari hayajatoka ila tayari baadhi ya Watanzania walipata nafasi ya kwenda kutazama mwili wake kwenye mochwari ya Hillbrow ambapo ameonekana ametokwa na damu nyingi sana puani.


Sehemu ulipohifadhiwa mwili wa Marehemu


Gharama za kusafirisha mwili wake kutoka South Africa ni zaidi ya $3500 ambazo bado haijawa rahisi kupatikana kwake, lakini juhudi zinafanyika ili kufanikisha.

Kumekua na habari mbili kubwa zinazoenea kwamba msanii rafiki aliepelekwa hospitali pamoja na Ngwea, yaani M2theP, amefariki na pia ripoti ya madaktari imetoka.

Zote hizo ni habari za uongo, ripoti ya daktari bado haijatoka na pia M2theP hajafariki dunia, ni mzima wa afya na amekua akiendelea vizuri.

Ameanza kufungua macho toka jana na hata kunyanyua miguu, kitu ambacho manesi wamesema ni matumaini kama akiendelea hivyo ndani ya siku tatu anaweza kuanza kuongea.


Baadhi ya Watanzania walikusanyika kupanga mipango ya kusafirisha mwili

Thursday, May 30, 2013

Ripoti ya Kutekwa, Kuumizwa Kibanda Hii Hapa

 
    UTANGULIZI:Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.Kama hiyo haitoshi, tukio la kutekwa na kudhuriwa kwa Kibanda limetokea mwezi mmoja tu baada ya Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu kupigwa risasi na polisi akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam kwa maelezo kuwa kimakosa polisi walidhani Matutu ni jambazi.Mazingira ya kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda yalitia wasiwasi kuwa upo uwezekano, na dalili zilionyesha kwamba waliofanya kitendo hicho cha kinyama hawakuwa wezi wala majambazi kutokana na ukweli kwamba licha ya kuwa na fedha zipatazo shilingi milioni tatu taslimu ndani ya gari, laptop, simu tatu za gharama (ipad, iphone na Blackberry), watekaji hawa hawakuchukua chochote baada ya kukamilisha uhalifu wao.Kibanda aliumizwa kwa kiwango kikubwa. Alitobolewa jicho la kushoto, akaumizwa vibaya kichwani kiasi cha kusababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya kichwa. Aling’olewa meno mawili na kucha mbili, tena bila gazi. Watekaji hawa, katika unyama wa ajabu kabisa, walimkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondokana nayo.Hali hiyo iliibua maswali mengi, watu wengi wakajiuliza na kutafuta sababu za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda kiasi hiki. Kutokana na kuwapo kwa maelezo mengi yanayotofautiana kuhusu tukio hilo, ikabidi Jukwaa la Wahariri Tanzania lifanye uamuzi.Katika kikao cha Machi 8, 2013 Jukwaa la Wahariri Tanzania liliunda TIMU ya watu watano na kuipa hadidu rejea za kufanya uchunguzi wa kihabari juu ya shambulio hilo kubaini limetokana na nini.Timu hiyo iliundwa kufuatia uamuzi wa Jukwaa la Wahariri kufanya uchunguzi huo na baada ya kukubalika kwa ombi la ruzuku ya kufanya uchunguzi huo wa kihabari kutoka Mfuko wa Vyombo Vya Habari Tanzania (TMF). Ruzuku ya TMF ililenga kiujumla kutumia tukio la Kibanda kuwa chanzo cha kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi na wahariri na kwamba kiwango cha matukio ya kuteswa, kupigwa na kuuawa kwa waandishi yanapungua kila mwaka. Timu hii imefanya kazi usiku na mchana kwa kwa zaidi ya mwezi. Timu imezungumza na wadau 26. Kati ya hawa yumo Kibanda mwenyewe, mke wake, ndugu zake, wasaidizi wake, waajiri wake wa zamani na wa sasa, viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola kutafuta ukweli wa jambo hili. Pia tumesoma matamko na habari zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya kati ya Machi 5, 2012 na Aprili 5, 2012 kwa nia ya kufanya ulinganishi wa taarifa tulizozipata kutokana na uchunguzi na habari zilizochapishwa baada ya kutekwa kwake.Vyombo vya dola akiwamo Waziri mwenye dhamana walikataa kuhojiwa wakisema kuna tume ya serikali inayofanya kazi hiyo na kwamba kuhojiwa kungeonyesha kutokuwa na imani na tume hiyo.Leo tunawasilisha muhtasari wa ripoti hii. Ripoti kubwa pamoja na viambatanisho vyake, itachapishwa na kuwekwa katika kitabu kimoja. Utaratibu mwingine wa kuchapisha habari ambazo hazijachapishwa kuhusiana na tukio hili (untold stories) pia utaandaliwa kwa ushirikiano na Jukwaa la Wahariri kwa nia ya kuieleza jamii maajabu juu ya kadhia hii.Tulipewa Hadidu Rejea ziafuatazo:





    HADIDU REJEA:1. Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya mashambulizi dhidi yake.2. Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.3. Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006), Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New Habari.4. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.5. Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika





    YALIYOJIRI KATIKA UCHUNGUZI:1.0. Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya mashambulizi dhidi yake.Timu ya uchunguzi ilitumia muda mwingi katika eneo hili, kubaini iwapo kulikuwapo viashiria, sababu au matukio ya wazi yenye mwelekeo wa kujitokeza kwa shambulio hili. Tuliangalia pia iwapo wapo watu au makundi yaliyokwishapata kuonyesha ishara kwa matendo au kwa kauli juu ya uwapo wa nia hii. Uchunguzi umebaini kuwa kuliwapo viashiria vingi, isipokuwa Kibanda au watu wake wa karibu hawakupata kufikiri kuwa huenda vingeweza kuleta madhara makubwa kiasi hiki kama ifuatayo:-





    1.1. Wiki tatu kabla ya Kibanda kuvamiwa, kutekwa na kuumizwa, gari la polisi aina ya gofu Na PT 180 liliwafuatilia kwa muda mrefu Absalom Kibanda na Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe likiwa limeegeshwa nje ya ofisi zao Sinza Kijiweni na baadaye likawafuatilia hadi Sinza Makaburini, ambapo walisimamisha magari yao na kuzungumza na polisi hao waliosema walikuwa wanatilia shaka magari yao. Baada ya kuzungumza kwa muda polisi waliondoka.



1.2. Usiku wa Februari 25, mwaka huu majira ya saa 09:00 usiku, Kibanda walivamiwa na watu walioingia kwenye uzio wa nyumba yao wakavunja kioo cha gari analotumia, lakini kioo kilipovunjwa ‘alarm’ ilipiga kelele, Kibanda akatoka nje na watu hao wakakimbia.

1.3. Kutokana na uvamizi huo, Kibanda na wapangaji wengine katika nyumba zilizopo kwenye uzio mmoja, waliona hatari ya kuvamiwa hivyo wakaanza mazungumzo na kampuni ya Ulinzi ya Kiwango, iliyowataka kufunga kamera za usalama na kuweka walinzi watano. Hadi Kibanda anatekwa, walikuwa hawajahitimisha mazungumzo na kampuni hii ya Kiwango.

1.4. Kuna askari anayefanya kazi Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) miezi minane kabla alipata kumpa Kibanda taarifa za kinteligensia, kuwa kulikuwapo mpango wa kumteka na kumuumiza. Taarifa kama hizo pia alipewa na wasamaria wanaofanya kazi katika Jeshi la Polisi. Kwa maneno yake Kibanda alisema:“Kuna rafiki yangu askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kama miezi minane au tisa hivi aliwahi kuniambia ‘unaandika sana usidhani kama watu wanakupenda. Chukua tahadhari hasa unapofika getini nyumbani kwako’. Tangu wakati huo nimekuwa nikichukua tahadhari sana.“Wiki mbili kabla ya tukio, niliwahi kuhisi kitu kama hicho [cha kuvamiwa] nikiwa getini. Nilipiga honi wakachelewa kuja kunifungulia, niliogopa sana. Hata nilipoingia ndani nilikuwa nimekosa raha kabisa.“Pia kuna rafiki zangu polisi waliwahi kuniambia kwamba ninatafutwa na kwamba watu wananifuatilia na ikibidi wanitengenezee ajali au kunifanyia kama Ulimboka au Kubenea.”

1.5. Ndani ya miezi mitatu mbele ya mlango wa ofisi yake Kibanda (Free Media Limited) ilikuwa mara kwa mara muda wa asubuhi anapofika ofisini anakuta damu. Haikufahamika kama damu hiyo ilikuwa ni ya binadamu, kuku, ng’ombe, kunguru au mbuzi, bali waliipuuza wakidhani ni masuala ya ushirikina. Mhariri Mtendaji wa sasa, Ansbert Ngurumo, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo.1.6. Mfanyakazi mwandamizi wa Kampuni ya New Habari anakofanya kazi sasa Kibanda ndani ya wiki mbili kabla ya kutekwa na kuumizwa kwake alipata kumwabia Kibanda maneno mazito mara tatu, na hapa tunamnukuhu Kibanda:“Aliniambia Danny Mwakiteleko [aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari] hakufa kwa ajali, bali alikufa kutokana na blood clotting (kuganda kwa damu). Hivyo ikitokea mtu ukapata ajali au ukapigwa na kuumizwa sana sehemu za kichwa hivi au tumbo, ni lazima madaktari wadhibiti sana blood clotting.“Na kweli, nilivyoletwa hapa Milpark hospitalini, madaktari walikuwa wananidunga sindano sita kila siku kwenye kitovu kuzuia blood clotting. .... (jina linahifadhiwa) aliniambia maneno haya mara tatu, katika mazingira yasiliyotarajiwa na kwa msisitizo ambao sikujua maana yake. Nasema .... (jina linahifadhiwa) naye achunguzwe kwa kina. Inawezekana kuna jambo analijua.”Ofisa huyu, alipishana dakika chache na Kibanda muda wa kutoka ofisini baada ya kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Real Madrid na Manchester united kumaliza nusu ya kwanza (half time). Dakika ishirini baadaye Kibanda alishambuliwa.

2.0. Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.2.1. Familia ya Kibanda na Kibanda Mwenyewe hawakuwa na wasiwasi wowote siku hiyo kwani hawakuwa na hisia wala wazo kuwa ungetokea uvamizi huo.

2.2. Kibanda alipopiga honi, mlinzi alisogea langoni kumfungulia. Ghafla akasikia kishindo kikubwa. Akasikia kelele za Kibanda akiomba msaada. Kijana huyu Baraka Ibrahim mwenye umri wa miaka 27, aliogopa. Aliogopa kwa mana hakuwa na silaha yoyote mkononi. Hakuwa na panga, kisu, rungu, wala filimbi. Kwa maneno yake anasema:“Nilivyoona ningefungua geti hata mimi ningekufa, nilikimbia kuwaamsha majirani. Sikuwa hata na namba ya simu ya mtu yeyote kati ya mabosi wangu ninaowalinda. Nilikuwa mimi tu, imani yangu na Mungu wangu.... kutokana na maisha naifanya hivyo hivyo tu. Vinginevyo milele nisingefanya kazi hii ya ulinzi.”Mlinzi huyo alikimbilia kwa majirani katika nyumba aliyoamini yumo mwanaume, lakini akaanza kumwamsha House Girl, ili house girl amwamshe baba mwenyenyumba. Kitendo cha kuamshana na kuwapa taarifa kilichukua dakika tano hadi saba, na ndani ya muda huo, Mlinzi anasema watekaji wa Kibanda walifanyafanya unyama na uasi huo na kuondoka ndani ya muda mfupi kiasi hicho. “Watu hawa wana mafunzo maalumu,” anahitimisha.

2.3. Mke wake alikwenda kazini asubuhi na kurejea nyumbani jioni, lakini tofauti na utaratibu wake wa kawaida ambapo huwa anaangalia televisheni sebuleni hadi Kibanda anaporejea nyumbani, siku hiyo alikwenda kuangalia televisheni akiwa chumbani na usingizi ukampitia. Anasema hakusikia honi wala tukio la Kibanda kutekwa. “Hii inanitesa sana moyoni. Najiuliza kwa nini siku hiyo tu sikukaa sebuleni? Kwa nini siku hiyo tu nimelala mapema kabla Baba Joshua hajarudi (machozi yanamlengalenga). Najiuliza sipati jibu.”2.4. Mmoja kati ya wasaidizi wawili wa nyumbani kwa Kibanda, alisikia kelele za Kibanda akiomba msaada. Alimwamsha mwenzake na kumwambia. “Nasikia Baba Joshua anapiga kelele kama amevamiwa hivi.” Mwenzake alimwambia “Unaota maana kuna kelele za mpira.” Siku hiyo kulikuwa na mechi kati ya Real Madrid na Manchester United.Ni kweli zilikuwapo pia kelele za wanaoshangilia mpira siku hiyo, hivyo Kibanda alipoomba msaada, hata waliosikia walidhani watu wanashangilia mpira. Binti aliwaamsha Angela na mwenzake, wakaenda sebuleni, wakakaa na kuchungulia dirishani, wakaona mwanga wa gari getini, lakini baada ya kutosikia kelele yoyote wakarejea kulala wakidhani siye. Lakini binti mmoja alibaki sebuleni. Baada ya muda jirani mmoja akampigia simu Angela kumweleza kuwa mumewe ameshambuliwa.2.5. Kibanda kwa upande wake, anasema alipofika getini, alipiga honi, ghafla akaona watu wawili wamesimama pembeni mwa gari lake na mtu wa tatu akiwa kwa mbali. Kisha akasikia kishindo kikubwa, akidhani wanataka kuiba gari, aliatokea mlango wa abiria na kuanza kukimbia huku akiita. “Mama Joshua nisaidieeeeee.”Katika kukimbia, aliteleza akaanguka. Huku watesaji wake wakisema mara tatu “Afande piga risasi.” Kibanda alijaribu kupambana, akashika rungu, akawahoji amewakosea nini hadi wampige kiasi hicho, lakini hawakumjibu lolote. Waliendelea kumpiga, hadi akapoteza fahamu. Hakujua jicho limetobolewa saa ngapi, meno yameng’olewaje na wala pingiri ya kidole chake imekatawaje. Ifuatayo ni sauti ya Kibanda mwenyewe. Inasikitisha ila tuwe wavumilivu na tuisikilize.

3.0. Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New Habari.

3.1. Mazingira ya kazi ndani ya New Habari (2006) Limited na Freemedia Limited, yanaacha maswali kadhaa yenye kustahili majibu. Kama ilivyoelezwa kwenye Hadidu Rejea Na: 1, ndani ya kampuni ya New Habari imekuwapo misuguano isiyo na afya kwa kazi ya Kibanda kama mwandishi na tasnia ya habari kwa ujumla.

3.2.Mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ni utata. Uhusiano katika chumba cha habari si mzuri. Ndani ya kampuni hawaaminiani na imefikia hatua wanatuhumiana kuwa huenda baadhi ya viongozi ndani ya New Habari wamehusika kumteka na kumuumiza Kibanda. Haya yameandikwa ndani ya mitandao ya kijamii, ikidai kwamba kiongozi mmoja ndani ya kampuni hiyo alihusika na utekaji wa Kibanda. Mkurugenzi wa Uhariri, Prince Bagenda anasema waliohusika kusambaza taarifa chafu dhidi ya kiongozi huyo wa New Habari wanatoka ndani ya kampuni hiyo.

3.3. Timu ya uchunguzi ilibaini kuwapo mgawanyiko mkubwa ndani ya New Habari (2006) Ltd kwa kuwapo kundi la ‘Habari Wazawa’ na ‘Habari wa Kuja’. Malalamiko mengi yanajikita katika msingi kuwa ajira hazitangazwi na watu wanaajiriwa bila kuzingatia sifa za kitaaluma.

3.4. Kibanda hakuhama Free Media kwa amani. Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda. Kwa maneno yake, anasema:“Nilihofu kuwa Mbowe anaweza kutugombanisha. Nikaona ni bora niondoke nisije nikagombana na Mbowe au Ngurumo.”Anasema alianza kupoteza mamlaka yake na kutoaminika kwa mwajiri wake baada ya kuandika makala kuhusu Abdulrahman Kinana ambayo kabla ya kuiandika hakuwa na wazo la kuondoka. Yaliyofuata baada ya makala hiyo, yalimshukuma aondoke.

4.0. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.

4.1. Uchunguzi ulifuatilia masuala mbalimbali ikiwamo miendendo ya watu waliotajwa kwa njia moja au nyingine kuhusinaa na tukio hili. Hata hivyo, karibu watu wote waliohojiwa, akiwamo Kibanda mwenyewe aliyeumizwa walimtaja kwa kutilia shaka mwenendo wa kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandano ya kijamii siku ya Machi 6, 2013.

4.2. Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick katika naye alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo. Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili, fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.

4.3. Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu wengi hasa baada ya kuleeza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kiwaida mwendo wake hauwezi kuzidi dakika 10. 4.4. Daniel Chongolo aliiambia timu kuwa alfajiri ya Machi 6, siku anayodai kutekwa Ludovick yeye alimuona eneo la Mabibo wakati anatoka Muhimbili. Chongolo alikwenda kituo cha polisi Mabibo na kupewa taarifa kuwa Ludovick alitoa taarifa polisi kuwa alikuwa ametekwa ila akarudishiwa mali zake zote. “Alipouliza amefuata nini polisi, akawambia kama raia mwema amefika kuandikisha kumbukumbu kwa nia ya kuonyesha kiwango cha uhalifu kinavyoongezeka nchini,” anasema Chongolo. Timu ya uchunguzi ilikataliwa kupitia leja ya polisi kama itakavyoelezwa hapa chini.

4.5. Pia taarifa za uchunguzi wa timu hii zinathibitisha kuwapo kwa utata juu ya madai ya kuibwa kwa simu za Joseph Ludovick, kwani simu yake ya tigo (inayodaiwa kuibwa) ilitumika saa 01:21 asubuhi siku ya Machi 6, 2013. Muda huu ofisi za Serikali na Kampuni ya Tigo zilikuwa hazijafunguliwa

5.0. Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika.

5.1. Uchunguzi umebaini kuwa maisha ya wanahabari yapo hatarini. Hatari hii inatokana na makundi mengi yenye masilahi kuwaona wanahabari wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa masilahi yao haramu. Kuna hatari kubwa inayowakabili waandishi wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

5.2. Uchunguzi umebaini kuwa usiri umepungua katika vyombo vya habari. Tofauti na zamani ambapo habari nyeti ziliandikwa kwa kuhifadhi majina ya waandishi wakitumia jina la MWANDISHI WETU. Simu hizi hata habari za kutisha waandishi wanaweka majina yao na hata wasipoweka, ndani ya vyumba vya habari vingi waandishi wapo tayari kutaja nani ameandika habari fulani.

5.3. Usaliti miongoni mwa waandishi wenyewe ndani ya vyumba vya habari unazidi kuongezeka na usipodhibitiwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi. Mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi anasema: “Hili ni jambo muhimu sana. Tuache usaliti vinginevyo wengi wataumia.”

5.4. Pia alishauri waandishi wa habari kurejea katika msingi wa taaluma, ambayo inawataka wao kuwa ndio wenye kuendesha vyombo vya habari badala ya kutegemea matakwa ya wamiliki au makundi yenye masilahi binafsi.

6.0. KILICHOBAINIKA:
6.1. Uchambuzi uliofanywa ni timu hii umebaini kuwa hoja nne zinazungumzwa kuhusiana na kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda. Hoja hizi ni:-(i) Kazi yake ya uandishi wa habari(ii) Uhusiano wa kisiasa na vyama au wanasiasa mbalimbali(iii)Uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi(iv) Vitendo vya rushwa.

6.2. Timu imejiridhisha kutokana na majibu ya wengi kuwa dhana ya mapenzi na rushwa, havina nafasi yoyote katika tukio hili. Wote waliohojiwa walieleza pasi na shaka kwamba suala hili la kushambuliwa na kuumizwa kwa kiwango kikubwa kwa Kibanda, halina uhusiano wowote na rushwa au mapenzi.

6.3. Kutokana na yaliyotajwa hapo juu kazi yake na siasa vikiunganishwa vimechangia kwa kiasi kikubwa kuvamiwa kwa Kibanda. Timu imebaini kuwa kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola na vyama vya siasa. Mchezo huu mchafu unaweza ukawa mwanzo wa kuumizwa kwa Kibanda na waandishin wengine.

6.4. Baadhi ya waliohojiwa walidai kuwa utekaji huu umefanywa na vyombo vya dola ukiwa sehemu ya mpango mkakati wa vyombo hivi kukihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vitendo vya ugaidi.6.5. Wanayataja matukio ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga, maandamano ya Morogoro na Mkanda anaodaiwa kurekodiwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare kuwa vililenga kukifanya CHADEMA kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja kama chama cha kigaidi ambacho kinateka watu na kinawaumiza.

6.6. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anadai kwamba mpango kama huo vyombo vya dola viliutumia kwa NCCR Mageuzi vikakisambaratisha, Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa udini kikapoteza mwelekeo na sasa vyombo hivyo vililenga kukifanya CHADEMA kionekane cha kigaidi mbele ya macho ya jamii ndiyo maana imerekodiwa mikanda kwa nia ya kuitumia kujenga hoja hiyo.

6.7. Wakati Mbowe akisema hayo, baadhi ya watu waliohojiwa wanadai kuwa CHADEMA kimepewa mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi kuwa kikitumia baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya watu maarufu nchini wakiwamo waandishi na wanasiasa, basi wananchi wataamini kuwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza kazi ya kuua wanaowapinga.

6.8. Kwa njia hiyo, inaelezwa kuwa hesabu za Chadema ni kuwa wananchi wataichukia CCM na Serikali yake na kukipa nafasi ya kuingia madarakani. Hapa kauli ya Chadema kuwa NCHI HAITATAWALIKA itakuwa imetimia.

6.9. Dhana nyingine iliyojitokeza ni kuwa wapo wafanyabiashara ambao wana vita binafsi, hivyo wanaamua kuumiza watu wasiowaunga mkono katika mipango yao na hilo ndilo limemkumba Kibanda, baada ya kuwa ameepusha mauaji ya mwandishi mmoja na aliyekuwa ameandaa mpango wa kuua mwandishi huyo hakuridhika hivyo akaamua amshughulikie Kibanda.

7.0. MAPENDEKEZO:Baada ya Timu kupata taarifa hizi na nyingine nyingi, inapendekeza yafuatayo:-

7.1. Taarifa hii ichukuliwe kama chanzo cha uchunguzi zaidi wa vyombo husika.7.2.

Yanahitajika marekebisho makubwa na ya haraka katika mifumo ya uendeshaji wa vyumba vya habari kwa nia ya kurejesha misingi ya uandishi wa habari inayokubalika.

7.3. Usalama wa wanahabari unapaswa kupewa kipaumbele na wamiliki, wanahabari wenyewe na jamii kwa ujumla. Hapa Timu inapendekeza yawepo mafunzo ya kuwawezesha wanahabari kutambua viashiria vya hatari na kuchukua hatua mara moja.

7.4. Kwa kiwango alichoumizwa Kibanda iwapo mwajiri wake asingejitolea kugharamia matibabu, hatujui hatima yake ingekuwaje leo hii. Tunapendekeza taasisi na mifuko mbalimbali inayojihusisha na masuala ya wanahabari kama Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kuanzisha mfuko wa pamoja utakaotumika kugharamia matibabu ya waandishi watakaoumia wakiwa kazini.

7.5. Tukio la kutekwa kwa Kibanda limeonyesha mwanga kuwa wahariri tumegawanyika mno. Habari zilizochapishwa katika magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii zimeonyesha haja ya kuwafanya wahariri kuwa kitu kimoja kwa kuondoa tofauti zao zisizo na masilahi kwa tasnia ya habari.

7.6. Kuna viashiria vingi kuwa kuelekea mwaka 2015 matukio ya waandishi kuumizwa au kutekwa yanaweza kuongezeka kutokana na wanasiasa na vyama kuwania madaraka huku wakitumia baadhi ya watumishi katika vyombo vya dola. Kwa mantiki hiyo, vyombo vya habari na waandishi wa habari wachukue tahadhari kuanzia sasa.

7.7. Taasisi za habari zifanye juhudi za makusudi kukutana na vyama viwili vya siasa vya CCM na CHADEMA haraka iwezekanavyo, kuzungumzia viashiria hivi vya hatari vinavyoelekea kuvuruga amani ya Tanzania.

8.0. HITIMISHO:Ni dhahiri kuwa kupigwa na kuteswa kwa Kibanda kumejiegemeza katika siasa na kazi yake, hali inayofanya makundi muhimu kuchukua wajibu wa msingi. Kwa upande wa Serikali ni muhimu kufuatilia viashiria katika taarifa hii kwa nia ya kupata ukweli zaidi na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya wahusika.Na kwa upande wa vyombo vya habari na taasisi za kihabari zinapaswa kutambua viashiria vinavyohatarisha usalama wa waandishi wa habari na wahariri na kutengeneza mazingira yatayokuwa salama zaidi kwa waandishi kufanya kazi zao.

9.0. SHUKRANI:

9.1. Tunapenda kulishukuru Jukwaa la Wahariri Tanzania, kwa kufanya uamuzi sahihi wa kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi huu ulioanza kuonyesha mwanga wa nini kilitokea.

9.2. Tunapenda kulishukuru Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushiriki kikamilifu na kuiwezesha timu hii kwa Rasilimali Watu na Mali kufanikisha kazi hii.

9.3. Tunapenda kuwashukuru Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) kwa uwezeshaji wa ruzuku, uliofanikisha kufanya uchunguzi wa kihabari uliohusisha kwenda nchini Afrika Kusini kufanya mahojiano na Kibanda. Uwezeshaji huo pia unahusisha kutengeneza mwongozo kwa waandishi wenye lengo la kuwaepusha na hatari za kiusalama.

9.4. Tunawashukuru Kibanda, mkewe Angela, wanafamilia, ndugu na jamaa wa Kibanda na wanahabari wote waliohojiwa kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Timu hii.

9.5. Tunawashukuru wahariri wote kila mtu kwa nafasi yake, kutokana na ushauri wa mara kwa mara mliotupatia katika kufanikisha uchunguzi huu.

10.0. WAJUMBE WA TIMU:Timu hii iliundwa na wajumbe watano ambalo ni:1. Deodatus Balile – Mwenyekiti2. Pili Mtambalike – Mjumbe3. Jane Mihanji – Mjumbe4. Tumaini Mwailenge – Mjumbe5. Rashid Kejo – Katibu

Mwisho.....
TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA IMEWASILISHWA NYUMBANI HOTEL - TANGA MEI 30, 2013

Source:Jamii Forums

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 31.05.2013


1 1c845
2 fdb2c
3 150c8
4 febf0
5 5e5ed
6 67f92
7 2a87d
8 0be47
9 e2ad8
10 cfcf1
11 5ff32
13 c0ecb

Hatimae K'Lyne Aweka Wazi Uhusiano Wake na Reginald Mengi Kwenye Twiiter

 Kumekuwepo na Minong'ono mingi lakini hapakuwa na ushahidi wa hili mpaka mwanadada huyo alipoamua kuanika hadharani kuwa mheshimiwa bwana Reginald Mengi ndiye baba halali wa mapacha wake wawili. Happy Birthday Mmili wa makampuni ya IPP bwana REGINALD mengi kwa kumiliki mtoto mkali TOP in town kimwana Jackline Ntuyabaliwe(K'lyne)  mapenzi hayana macho siku zote.

Hii ndio Tweet ya K'lyne kwa mpenzi wake Mh. MENGI

BUNGENI: Vurugu zasababisha Bunge kuahirishwa.


Kufuatia hotuba ya Wenje bungeni kutuhumu chama cha cuf kuwa ni chama cha kishoga, mbunge wa CUF amesimama na kuwaita chadema ni wehu, wahuni, wazushi, mashoga na kwamba wameidhalilisha cuf...

Mbunge huyo wa CUF ameomba spika achukue hatua za dhidi ya chadema asipofanya hivyo cuf watachukua hatua dhidi ya Chadema na bunge..

Kumetokea vurugu bungeni ambapo spika ameliahirisha bunge hadi jioni.

Hiki ni Kipande cha hutuba hiyo ambacho nimekitoa Jamii Forums:
"Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.
Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.
Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo "

Full Interview P-Funk Akizungumzia Kifo Cha Marehemu Albert Mangwair

Tuesday, May 28, 2013

KIJANA ANASWA AKIUZA UUJME WA MTU....POLISI WATIA MBARONI

Jeshi la polisi nchini malawi wanamshikilia kijana mmoja baada ya kumkuta akiuza sehemu ya siri ya mwanaume.
Kijana huyo mwenye miaka 24 alikamatwa baada ya wananchi kutoa ripoti kituo cha polisi kuwa kunamzee kalala relini huku akiwa anatokwa damu nyingi 
 Polisi walifika eneo la tukio na kumkuta mzee huyo akiwa hoi na kuamua kumkimbiza hosipitali.

Baada ya kufikishwa hosipitali, madaktari  gundua kuwa mzee huyo alikuwa amejeruhiwa kwa kukatwa sehemu zake za siri...

Madaktari hao walilipoti kwa maofisa hao wa polisi na ndipo msako mkali ulipo pita katika wilaya ya Lakeshore mjini Salima na polisi hao kufanikiwa kumtia mbaroni kijana huyo baada ya kumkuta  akiwa katika gesti bubu akijaribu kuuza uume huo kwa dola za kimarekani 360.
                            Mtuhumiwa Samuel Banda
Polisi walisema mtuhumiwa Samuel Banda alikamatwa na kiungo hicho ambacho alikuwa amekifunga katika karatasi nyeupe.

Mtuhumiwa alikiri kuwa huwa anauza viungo mbalimbali vya binadamu kwa wafanya biashara maarufu nchini humo ambao wanaamini wakivipata viungo hivyo huwasaidia katika biashara zao na huwaongezea utajiri.

Monday, May 27, 2013

FREEMAN MBOWE AFUNIKA KATIKA MKUTANO WA HADHARA KANDA SONGEA. .... ONA MAKUBWA YALIYOJILI ...

Mwenyekiti wa Chana cha Chadema - CDM - Taifa na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Mhe Freeman Mbowe, (Mb.) akihutubia umati wa watu katika viwanja vya Shule ya Msingi Matarawe manispaa ya Songea wakati wa kampeni ya Chama hicho kuzindua kanda ya kusini leo. (Picha na Juma Nyumayo)
Mhe. Freeman Mbowe, akisisitiza umuhimu wa wananchi wa mikoa ya Kusini, hasa mkoa wa Ruvuma ambao hauna Mbunge wa Upinzani hata mmoja kujiunga na vita ya kupambana na ufisadi na kunyimwa haki wananchi kwa kujiunga na upinzani katika viwanja vya Shule ya Msingi Matarawe Manispaa ya Songea leo.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kusikiliza mkutano wa uzinduzi wa Kanda ya Chadema Kusini mwa Tanzania mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma leo ambapo Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho alihutubia.
Nidhamu kwa kwenda mbele watu wa makundi na rika tofauti wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe, katika Mkutano wa kihistoria wa Kufungua kanda ya chama hicho uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Matarawe leo.
Mpambe wa Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe, (mwenye nguo ya mabaka meusi) aliyesimama nyuma ya kiongozi huyo, akiwa makini kuangalia usalama wakati akihutubia wananchi katika viwanja vya shule ya Msingi Matarawe leo kuhusu vita dhidi ya mafisadi na umuhimu wa wananchi hao kujiunga na Chadema. Chama hicho kimekamata kata tano nafasi za udiwani Jimbo la Songea mjini zikiwa ni Kata ya majengo, Misufini, Mfaranyaki, Bombambili, Lizaboni na Bombambili. Mkutano huo uliopigwa marufuku na baadae kuruhusiwa kwa hekimas za Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mhe Said Thabit Mwambungu kutokana na kukubaliana na vingozi wa Chadema kutofanya maandamano.Tendo hilo limewafanya chadema leo kumsifu mkuu wa mkoa huyo hadharani kwa maauzi yake. (

Sunday, May 26, 2013

Alalamikia anayedai kuleta miradi ya umeme kwa fedha binafsi

MBUNGE wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM) ameliambia Bunge kwamba kuna mtu katika Jimbo la Bukoba Vijijini anayejitapa kwa wananchi kwamba miradi ya umeme inayotekelezwa jimboni humo inatokana na fedha zake.
Alisema hatua hiyo inawafanya wananchi kuichukia Serikali kwa kudhani kwamba haitekelezi miradi ya maendeleo bali miradi hiyo inatekelezwa na watu binafsi.
Akichangia kwenye mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni, Rweikiza alisema mtu huyo (bila kumtaja kwa jina) amekuwa akipotosha ukweli wa miradi inayotekelezwa na Serikali ya kusambaza umeme vijijini kupitia Wakala wa Umeme Vijijini (REA) akisema anaijenga yeye.
“Mheshimiwa Spika kwa kuwaeleza wananchi kwamba miradi hii inajengwa na mtu binafsi kunawafanya wananchi kudhani kwamba Serikali haiwajibiki kwao, nafurahi sasa Waziri kupitia hotuba yake ameeleza ukweli kwamba miradi hii ya umeme inatekelezwa na Serikali na si mtu binafsi na wananchi wajue kwamba mtu huyu ni mwongo anawadanganya wananchi,” alisema.
Katika kusambaza umeme vijijini na hivyo Serikali inawajibika kuongeza fedha zinazotengwa ili kupeleka umeme katika maeneo ya vijijini ili kuchochea maendeleo katika maeneo hayo hatua itakayosaidia pia kukuza Pato la Taifa.
Alisema pamoja na jitihada hizo za kusambaza umeme katika vijiji vya Bukoba Vijijini lakini bado yapo maeneo ambayo umeme unapita juu lakini chini wananchi wakosa umeme hatua ambayo inaathiri maendeleo kwa wananchi wa vijiji hivyo na hivyo ni lazima REA isambaze umeme katika vijiji hivyo haraka.
Akizungumza nje ya Bunge, Rweikiza alimtaja mtu huyo anayepotosha wananchi kuwa miradi ya umeme ya Serikali ni yake amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo na amewahi pia kuwa Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne (Nazir Karamagi ) akidai anataka kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Fezza Kessy Awa Mtanzania wa Pili Kuingia Nyumba ya Big Brother Africa


Baada ya Kuwa na Tetesi kuwa Fezza Kessy Atakuwa ni mmoja wa wakilishi wa Tanzania Big Brother Africa ...leo hii Amekuwa ni Mmoja kati ya Watanzania Wawili Wanao Iwakilisha Tanzania katika Jengo Hilo....So Tuna Wawakilishi Wawili Nando na Fezza Kessy...

MWANAMKE MCHAWI ADONDOKA KANISANI AKIWA UCHI WA MNYAMA JIJINI DAR


Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.

Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
 
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

Ilidaiwa kuwa muda mfupi baada ya maombi kuanza, katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke huyo aliruka kupitia dirishani akapotea na kuacha waumini vinywa wazi.

 
Habari zilidai kuwa kuna baadhi ya watu walimuona kwenye paa ya nyumba ya watu waliojenga karibu na kanisa hilo, hali iliyozidi kusababisha mkusanyiko mkubwa wa watu wakiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) waliokuwa wakimshangaa.
 
Wakati taharuki hiyo ikiendelea, mwanahabari wetu alitonywa kuwepo kwa tukio hilo ambapo aliwasha ‘tukutuku’ yake na kuwahi eneo la tukio.
Akizungumzia tukio hilo, mmoja wa viongozi wa kanisa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Octavian Mahembe alikuwa na haya ya kusema: 
 
“Nakumbuka kulikuwa na waumini wengi kanisani, walikuja kwa ajili ya maombi, huyo mwanamke naye alikuja hapa kama waumini.

“Ilipofika saa 5:00: asubuhi watu wakawa wanasubiri maombi, baadaye nabii naye akawa amefika na kuanza kutoa maombi. Baada ya maombi kuanza, yule mwanamke alianza kuhangaika, akawa anahamahama, hatulii sehemu moja.

“Watu waliokuwa wanataka kuombewa waliambiwa wapite mbele.


“Yule mwanamke alikurupuka na kurukia ukuta wa futi sita na nusu, akadondoka nje.

“Nabii alisema afuatwe ili aombewe, alidai kwa kuwa si mtu mwema ni hatari na anaweza kuliangamiza kanisa na waumini kwa jumla kwani alikuwa na nguvu za giza.

“Alipochukuliwa akapelekwa kwa Nabii, akaombewa sala ya toba huku akikataa kwa kusema hana dhambi.
 

“Aliendelea kuombewa na baada ya maombi alitoka nje kupitia mlangoni. Akiwa nje alivua nguo na kubaki na ile ya ndani tu, akapanda juu ya paa la nyumba jirani na kanisa, akarukia nyumba nyingine juu kwa juu bila kushuka.
 

“Hakuishia hapo, akawa amerukia mti huku akionekana kama mtu wa ajabu kiasi kwamba hata watu wengine hawawezi kufanya yale aliyokuwa akiyafanya.

“Watu wengi walikusanyika wakiwemo polisi na wanajeshi. Baada ya kupotelea mitini, ghafla kilisikika kishindo kanisani baada kudondoka eneo hilo.

“Baadaye alipelekwa ofisi ya serikali ya mtaa kwa usalama wake kwani watu walitaka kuchukua sheria mikononi wakidai ni mchawi,” alimaliza kusimulia kiongozi huyo wa kanisa.

Hata hivyo, habari nyingine zilidai kwamba kabla ya mwanamke huyo kupelekwa serikali ya mtaa, wakati akiombewa alikuwa akitangaza mambo mengi aliyokuwa akiyafanya yasiyoeleweka kwa watu wasiojua mambo ya kilozi.

Mwandishi wetu hakuishia hapo, alikwenda hadi ofisi za serikali za mtaa kutaka kujua kama mwanamke huyo alifikiswa hapo na sehemu alipo kwa sasa.
 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Salasala, Monica Timba alikiri kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa siku hiyo hakuwepo ofisini lakini alipigiwa simu na mkazi wa eneo lake kujulishwa juu ya tukio hilo.
 

“Niliambiwa kuna vurugu kubwa katika mtaa wangu na kwamba kulikuwa na mchawi amedondoka kanisani,” alisema mwenyekiti huyo.
 

Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa  baada ya kupewa taarifa hiyo alimpigia simu mtendaji wake, Ramadhan Juma ili mwanamke huyo aokolewe na walifanya hivyo.

Alisema kuwa baadaye mwanamke huyo alipelekwa kituo kidogo cha polisi kilichopo eneo hilo cha Mtongani. 

VIKONGWE WATATU WAUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA


MAUAJI ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja kama Kuku kisha kuwachoma moto vikongwe watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha na vitendo vya kishirikina. 
 Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vikongwe hao kwa tuhuma kwamba walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga na kuwatafuna kumaliza hasira zao.
 Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua kijana huyo hivi karibuni.
Kijana huyo alikufa kwa kugongwa na gari, lakini dereva aliyemgonga alidai hakuona kama alimgonga mtu ila mbwa na pia inaelezwa  tangu azikwe kijana huyo alikuwa akirejea kwa mkewe na kumuita nyakati za usiku pamoja na kusumbua familia yao akitaka apewe chakula na ndipo wanafamilia hao walipoamua kwenda kwa mganga kuchunguza tukio hilo. 
 Wakiwa kwa mganga,wanafamilia hao walitajiwa majina ya wanakijiji watatu wa kijiji hicho ambao hata hivyo walitoroka kwenda vijiji vya jirani pamoja na familia zao kabla ya usiku wa leo kuvamiwa walipokuwepo na kuangushiwa adhabu hizo za kinyama. 
Wa kwanza kushambuliwa na kuuwa ni bibi aitwaye Bi Mgala ambaye alikimbilia kijiji cha jiorani kwa rafiki yake aitwaye Bi Laya, ambapo walimkata miguu yote miwili na kumtenganisha kichwa na kiwiliwili kabla ya kumchoma moto ambapo hata hivyo kitu cha ajabu ni kwamba ziliungua nguo zake tu huku mwili ukiwa upo vile vile. 
Baadaye walimgeukia Bi Laya aliyekuwa akitaka kuwatoroka na kumfanyia unyama kama rafikie kwa kosa la kumhifadhi Bi Mgala kwa kuamini huenda wanafanya shughuli za kishirikina pamoja na baadaye kurudi Kasaula na kumnasa Bi Chausiku na kumfanyia kama walivyowafanyia ajuza hao wengine kisha kuchoma nyumba tatu. 
 Bibi wa tatu wanayemtuhumu pia kwa ushirikina, ametimka kijijini hapo, lakini nyumba yake imeteketezwa pamoja na kuku waliokuwa wakiwafuga kuporwa na watu hao na kutumia moto waliouwasha katika nyumba hizo kuwachoma na kuwala kwa hasira. 
Kamanda wa Polisi wa Bunda, Mika David Nyange amethibitisha juu ya tukio hilo la kusikitisha na kwamba wanedelea na upelelezi kwa nia ya kuwasaka waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mikononi.

UPDATE: TRENI YAUA UKONGA- MOSHI BAR MUDA HUU




Muda mfupi auliopita treni imegongana na gari aina ya RAV4 na dereva (mwanaume)amekufa muda huu na abiria(mwanamke) yu mahututi.

Thursday, May 23, 2013

Kikwete: Hata kama Mtu anaechochea Wananchi Ana Pembe Tutayakata

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani mh Jakaya Kikwete leo akihutubia ktk Mkutano wa CCM mkoani Dodoma huku akionekana mwenye hasira, amesema kua Serikali haipo tayari kuwavumilia wale wote wanachochea wananchi kufanya Vurugu baada ya Waziri wa Nishati na Madini kuwasilisha hotuba yake leo.

Alisema kua wapo watu Viongozi wanaochochea kwa Maslahi ya kisiasa na kwamba watahakikisha wote wanakamatwa iwe wapo ndani au nje ya nchi na kuwafikisha ktk vyombo vya Sheria.
Akiongea kwa hasira alisema kua Hata kama anaechochoe Wananchi kufanya Vurugu Ana PEMBE watamkamata na kumkata hizo Pembe.

Source: TBC1 TAARIFA YA HABARI.

Monday, May 20, 2013

SPIKA WA BUNGE AAMURU KUFUTWA KWA HOTUBA YA SUGU ILIYOSABABISHA BUNGE LISITISHWE ASUBUHI




Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mh Anne Makinda, ameamuru kambi ya upinzani kuyaondoa maneno yote yaliyomo kuanzia ukurasa wa kwanza mpaka wa 14 katika hotuba rasmi ya Kambi ya upinzani iliyosmwa na mbunge wa Mbeya Mjini, Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu,’ ambaye ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Mh. Makinda ametoa amri hiyo baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kujadili hotuba hiyo na kubaini kuwa ina kauli za uchochezi; na kusema kuwa kuwa Bunge sio sehemu kugombanisha wananchi, hivyo maneno yote ya uchochezi hayaruhusiwi.
 
Katika hotuba hiyo, Mh. Mbilinyi aliishutumu serikali kuhusika na kuteka nyara waandishi wa habari, kauli iliyopelekea Spika Makinda kuahirisha Bunge.


SEHEMU YA HOTUBA  HIYO:
MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013)
1. UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,


Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora, linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.’


Mheshimiwa Spika,


Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala. 
Tanzania imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho, kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. 
Tanzania sio nchi inayoandaa vijana wake tena. Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa. Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’ ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!


2. UHURU WA UHARIRI NA USALAMA WA WANAHABARI


Mheshimiwa Spika,


Kwa masikitiko makubwa, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inalitaarifu Bunge lako tukufu kwamba sasa Tanzania imeingia rasmi katika orodha ya fedheha (The List of Shame) ya mataifa ambayo taaluma ya habari ni taaluma ya hatari kwa wale wote wanaoitumia kama sehemu ya wajibu wao kwa taifa na kama ajira yao. 
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari Ulimwenguni (the Committee to Protect Journalists - CPJ) iliyotolewa mwaka huu 2013, kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa CPJ mwaka 1992, Tanzania imeingizwa kwenye orodha ya nchi 20 ambazo ni hatari kwa waandishi wa habari kufanya kazi zao kutokana na hatari ya kuuwawa kwa mwaka 2012 (20 Deadliest Countries in 2012). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilishikilia nafasi ya 7 ulimwenguni kati ya nchi 20 zinazoongoza kwa kuhatarisha maisha ya waandishi wa habari.

Mheshimiwa Spika,


Kwa mujibu wa taarifa ya CPJ, tishio kubwa kwa waandishi wa habari duniani ni kuuwawa kwa kutekwa na kuteswa na/au kutishiwa maisha. Aidha, Serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama ni washiriki wakubwa wa mauaji ya waandishi wa habari. 
Kwa mujibu wa takwimu za CPJ, kati ya waandishi waliouwawa mwaka 2012, karibu ya 20% waliuwawa ama na maafisa wa serikali au na majeshi yake. Karibu idadi hiyo hiyo ya waandishi wa habari waliuawa kwa sababu ya kufuatilia taarifa za kiuchunguzi na za hatari. Taarifa hiyo inaonyesha kwamba hadi kufikia Aprili 2013, waandishi wa habari wapatao 30 tayari wamekwishauawa ulimwenguni wakati wakitimiza wajibu wao; wakati mwaka 2012 waandishi wa habari 103 waliuwawa ulimwenguni kote.

Mheshimiwa Spika,

Taarifa ya CPJ inaungwa mkono na ushahidi wa matukio mengi yanayodhihirisha kwamba maisha ya waandishi wa habari wa Tanzania yako hatarini kutokana na vitendo na vitisho kutoka kwa Serikali na watendaji wake ambao hawataki kusikia ukweli dhidi yao ukianikwa hadharani. Kudhihirisha kauli hii tunaomba kumnukuu mwanahabari mahiri na mmoja wa wahanga wa vita dhidi ya wanahabari na uhuru wa habari hapa nchini, Mzee Ndimara Tegambwage:

“Mwaka 2006, waliojiita wananchi wakazi wa jiji la Mwanza, walikusanywa na wenye uwezo kufanya maandamano makubwa kwa walichoita ‘kupinga mwandishi Richard Mgamba kuandika uongo’ na kudai kwamba alikuwa Mkenya na ‘siyo raia wa Tanzania.’ Desemba 2009, mwandishi Frederick Katulanda wa Mwanza, alivamiwa nyumbani. Wavamizi walikuwa wakipaza sauti na kudai kuwa ana nyaraka za akaunti za benki za Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Walikuwa na mapanga. Walikuwa wakichagizana kwa kusema, “Kata kichwa! Kata kichwa!” Waliondoka na mafaili. Walimwachia kilema mguuni na makovu mikononi.


“Mwezi Septemba, 2010 wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, katika eneo la Nyambiti, Jimbo la Sumve wilayani Kwimba, mkoani Mwanza, mwandishi Frederick Katulanda alivamiwa na kupigwa na watu wapatao 15 waliojiita “Green Guard” - wa “chama cha kijani.” Katika “kumshughulikia,” Katulanda anasema, walikuwa wakionyesha kuwa na ujuzi mkubwa wa judo na karate huku wakidai kuwa anawaandika ‘vibaya’ Chama Cha Mapinduzi (CCM).


“Mwaka 2011 mwandishi Richard Massatu alikutwa amekufa katika eneo la Igoma, jijini Mwanza. Vyombo vya habari viliripoti kuwa macho yake yalikuwa yametobolewa na kuwekwa gundi aina ya super glue; mguu wa kushoto na mbavu vilikuwa vimevunjika. Vyombo vya habari viliripoti kuwa Massatu aliyekuwa mmiliki na mhariri mkuu wa gazeti la Kasi Mpya (sauti ya umma), alionekana mara ya mwisho usiku wa kifo chake akiwa na maofisa wa polisi na usalama katika baa iitwayo Cross Park katika eneo la Igoma.


“Tarehe 3 Januari, maiti ya mwandishi Issa Ngumba iliokotwa katika pori la mlima Kajuruheta, kijiji cha Mhange, wilayani Kakonko katika mkoa wa Kigoma.Ngumba alikuwa mwandishi wa habari wa Redio Kwizela. Tangu mwezi uliopita Machi, mwandishi wa habari Erick Kabendera anayeishi Dar es Salaam, anaishi kwa wasiwasi. Wazazi wake waishio Bukoba, wamehojiwa na ‘ofisa usalama’ kwa kile kilichoitwa ‘uhalali wa uraia wao.’


“Kuuwawa kwa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV, John Lubungo ambaye alikuwa mfuatiliaji mahiri wa habari zinazohusu wafanyabiashara au biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo inadaiwa kufanywa na watu wakubwa nchini, wakiwemo vigogo serikalini. 
Kuna orodha ndefu ya waandishi wa habari waliotishwa na wanaoendelea kutishwa; waliopigwa na polisi na askari magereza (Ukonga, Dar es Salaama) kwa tuhuma mbalimbali; waliotishiwa maisha kwa simu na hata kwa kufuatiliwa na watu wasiowafahamu.”

Kwa sababu ya uadilifu na kutopenda kujikweza, Mzee Tegambwage hakutaja shambulio la tindikali na mapanga dhidi yake na mwandishi mwenzake Saed Kubenea wa gazeti la Mwanahalisi, ambalo baadae lilifungiwa na Serikali hii ya CCM.


Mheshimiwa Spika,


Katika Maoni yake wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria ya tarehe 3 Mei mwaka huu, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilielezea kwa kirefu jinsi ambavyo Serikali hii ya CCM imekuwa tishio kwa maisha ya waandishi wa habari na kwa uhuru wa habari katika nchi yetu. 
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilirejeaRipoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi Iliyoteuliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Kuchunguza Mazingira Yaliyopelekea Kuuawa kwa Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi Septemba 2, 2012 Katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), taasisi mbili huru zinazojihusisha na masuala ya habari Tanzania.

Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, matokeo ya uchunguzi wao “... yanadhihirisha bila wasi wasi kwamba polisi kwa makusudi waliwavurumisha waandishi waliotoka Iringa wakati wakikusanya habari za shughuli za CHADEMA katika kijiji cha Nyololo.
 Zaidi ya hapo, Daudi Mwangosi mwenyewe aliuawa akiwa mikononi mwa polisi huku wakisimamiwa moja kwa moja na Kamanda (wa Polisi wa Mkoa wa Iringa SACP Michael) Kamuhanda.” Ripoti hiyo inaelezea jinsi Marehemu Mwangosi alivyouawa: “Alipoangalia nyuma, Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi wakimpiga mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe wa Iringa, Godfrey Mushi.... Wakati mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi, marehemu Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi Mushi kwa kuwa alikuwa mwandishi tu. 
Polisi hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye tayari alikuwa amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na wakamgeukia Daudi Mwangosi mwenyewe, wakampiga kwa nguvu mpaka akapoteza fahamu.”

Hata amri ya Mkuu wa Kituo cha Polisi Mafinga Mwampamba kuwataka askari polisi waache kumpiga marehemu Mwangosi haikusikilizwa na askari hao. Ili kujiokoa, marehemu Mwangosi alimkumbatia OCS Mwampamba na “baadaye kumwangukia miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi.” 
Kwa mujibu wa Ripoti ya MCT/TEF, “picha za mgando zinaonyesha polisi mmoja akipiga bomu la machozi tumboni mwa marehemu Mwangosi kwa karibu kabisa.” Bomu hilo liliusambaratisha mwili wa marehemu Mwangosi aliyekufa papo hapo. Kwa sababu marehemu Mwangosi alikuwa chini ya miguu ya OCS Mwampamba, “naye pia alijeruhiwa vibaya.”

Mheshimiwa Spika,


Sio MCT/TEF pekee zilizofanya uchunguzi wa mauaji ya Marehemu Mwangosi. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nayo ilitoa Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ya Uchunguzi wa Tukio Lililopelekea Kifo cha Daudi Mwangosi Kilichotokea Septemba 2, 2012 Kijijini Nyololo, iliyobaini kwamba Marehemu Mwangosi “... alizingirwa na askari, aliteswa na hatimaye ... alipigwa bomu na kufa papo hapo.” Aidha, kwa mujibu wa Taarifa hiyo, “... 
Tume imejiridhisha kuwa tukio la lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.” Taarifa ya Tume inafafanua kuwa, “... 
Tume imejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki ... ya kuishi, haki ya kutoteswa na kupigwa, haki ya usawa mbele ya sheria na haki ya kukusanyika na kutoa maoni.”

Mheshimiwa Spika,

Pombe si Maji: Inakuwaje Mtu Ulewe Kiasi Hichi?

                              Pombe si Maji: Inakuwaje Mtu Ulewe Kiasi Hichi?

Obama to Visit S’Africa, Tanzania, Rwanda, Considers Stopover in Nigeria-Snubs Kenya Again!

President Barack ObamaBy Paul OhiaPresident Barack Obama of the United States is billed to begin his second tour of Africa at the end of June with visits to South Africa, Tanzania and Rwanda.He will however make a stopover in Nigeria, during which he will hold bilateral discussions with President Goodluck Jonathan and other top government officials.The initial plan for the African tour was for Obama to spend two days in Nigeria, but owing to insecurity occasioned by the terrorist activities of the Islamic militant group, Boko Haram, the plan was reviewed and he is now expected to spend a few hours or one day in the country.Sources from the presidency added that security situation during Obama’s visit would be paramount and if there is any reason to doubt Nigeria’s unpreparedness to host the US president, his visit to the country might be cancelled outright.Obama’s maiden visit to Africa took him to Ghana in July 2009 during which he met with President John Atta Mills, now deceased, and delivered a speech at the Ghanaian parliament in addition to touring a former departing point of the trans-Atlantic slave trade, the Cape Coast Castle.The non-inclusion of Nigeria on his itinerary in 2009 was widely regarded as a snub and a subtle criticism of the country’s leadership, a perception, which the then Secretary of State, Mrs. Hillary Clinton, dismissed.She had said Obama’s choice of Ghana was “meant to tea-up” US relationship with sub-Saharan Africa, and the choice should not be interpreted in any other way.During his visit, the two nations are expected to discuss issues centred on trade relations, security and human rights.

Polisi Wakamatwa na Bangi Gunia 18 Wakisafirisha na Gari ya Mkuu wa Polisi

Siku chache baada ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwakamata askari 16 wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya magendo, askari wengine wawili wa jeshi hilo wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa na shehena kubwa ya bangi wakiisafrisha kwenda nchini Kenya.
Askari hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu saa nne usiku eneo la Kilemapofu, Wilaya ya Moshi Vijijini wakiwa na magunia 18 ya bangi ambayo walikuwa wameyapakia kwenye gari la Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoani Arusha aina ya Toyota Land Cruiser lenye namba PT 2025.
Akithibitisha kukamatwa kwa askari hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema askari hao walikuwa wakipeleka bangi hiyo Wilaya ya Rombo kwa mfanyabiashra mmoja ambaye hakutaka kumtaja jina lake.
Kamanda Boaz aliwataja askari waliokamatwa na wanashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi katika mji mdogo wa Himo kuwa ni F.1734 Koplo Edward (dereva) wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mkoani Arusha na G.2434 Konstebo George wa kituo cha polisi Ngarenanyuki Wilaya ya Arumeru.
Alibainisha kuwa kukamatwa kwa askari hao kunatokana na operesheni ya kukabiliana na dawa za kulevya inayofanywa na polisi katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Alisema operesheni hiyo imefanyika kikamilifu katika Mkoa wa Arusha uliokuwa ukitumika kupitishia bidhaa hiyo, na sasa wahusika wameamua kuutumia Mkoa wa Kilimanjaro.
“Baada ya kuwahoji askari wale, walidai kuwa walikodishwa na mfanyabiashara huyo kuipeleka bangi hiyo wilayani Rombo tayari kwa kusafirishwa kwenda nchini Kenya ambako inaaminika kuna soko kubwa,” alisema.
Kamanda Boaz alisema hivi sasa polisi wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na wenzao wa Arusha wanafanya uchunguzi kubaini mtandao wa askari hao unaojihusisha na vitendo haramu.
Aliongeza kuwa hatua inayofuata kwa askari hao ni kufunguliwa mashtaka ya kijeshi na iwapo watakutwa na hatia watafukuzwa kazi kisha watafikishwa katika mahakama za kiraia.
Kamanda Boaz alibainisha kuwa kwa kawaida askari wanapotoka mkoa mmoja kwenda mwingine hupatiwa kibali maalumu cha kusafiria (Movement Order).
Alisema kibali hicho husaini kila mkoa ambao askari husika hupita, lakini waliokamatwa na bangi hawakuwa nacho.
Kamanda Boaz alibanisha kuwa kwa hali ilivyo askari hao waliondoka na gari la mkuu wa FFU bila kumpa taarifa wala kupata kibali chake.
Tanzania Daima limedokezwa kuwa askari hao wamekuwa wakisafirisha bangi hiyo mara kwa mara kupitia mji huo wa Himo bila kukamatwa kutokana na gari lao kuwa na namba za kijeshi, hivyo kuwa vigumu kwa askari wenzao kuwatilia shaka.
Taarifa zaidi zimedai kuwa kukamatwa kwa askari hao kulitokana na gari lao kupata hitilafu katika eneo hilo la Kilemapofu, na ndipo askari wa doria walipofika kwa lengo la kutoa msaada kwa wenzao, lakini ghafla walisikia harufu ya bangi.
Mtoa taarifa aliyezungumza kwa sharti la kutotaka jina lake litajwe, alisema baada ya askari hao kusikia harufu ya bangi waliwaarifu viongozi wao waliowaamrisha walifanyie upekuzi gari hilo sambamba na kuwaweka chini ya ulinzi askari wote waliokuwamo.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa katika upekuzi huo walibaini uwepo wa magunia 18 ya bangi yaliyolengwa kupelekwa nchini Kenya.
Kilibainisha kuwa baada askari hao kukamatwa, mmoja wao alisikika akiongea na mtu aliyemuita bosi kumuarifu kukamatwa kwao.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa bosi aliyearifiwa tukio hilo alihoji imekuwaje wakakamatwa kizembe namna hiyo.
Kilidokeza kuwa bosi huyo alimhoji aliyempigia simu kuwa wamebaki na shilingi ngapi ili wawape rushwa polisi waliowakamata.
“Bosi aliambiwa kuna laki tano, naye akawaambia wawape fedha hizo zote, lakini kwa bahati mbaya hawakufanikiwa,” kilisema chanzo chetu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, hakukiri wala kukanusha kuwapo kwa taarifa za kukamatwa kwa askari wake.
Tanzania Daima lilitaka kujua Jeshi la Polisi mkoani Arusha limechukua hatua gani dhidi ya askari hao ambapo kamanda Sabas alisema hayupo katika nafasi nzuri ya kulizungumzia jambo hilo kwa kuwa yupo hospitalini.