Friday, May 31, 2013

update za Kifo chake Ngwea By Millard Ayo

Kifo chake Ngwea
By Millard Ayo | Fri, 31 May 2013Mpaka sasa bado unaendelea utaratibu wa kusafirisha mwili wa Marehemu Albert Mangwea kutoka Johannesburg, South Africa, kutoka kwenye mochwari ya serikali ya Hillbrow.

Mangwea alifariki dunia 28 May akiwa Johannesburg, alipokuja kufanya show ambazo Watanzania wa huku wanasema mara ya mwisho kuonekana kwenye stage ilikua wiki tatu zilizopita.

Bado chanzo cha kifo hakijajulikana na bado pia majibu ya uchunguzi wa Madaktari hayajatoka ila tayari baadhi ya Watanzania walipata nafasi ya kwenda kutazama mwili wake kwenye mochwari ya Hillbrow ambapo ameonekana ametokwa na damu nyingi sana puani.


Sehemu ulipohifadhiwa mwili wa Marehemu


Gharama za kusafirisha mwili wake kutoka South Africa ni zaidi ya $3500 ambazo bado haijawa rahisi kupatikana kwake, lakini juhudi zinafanyika ili kufanikisha.

Kumekua na habari mbili kubwa zinazoenea kwamba msanii rafiki aliepelekwa hospitali pamoja na Ngwea, yaani M2theP, amefariki na pia ripoti ya madaktari imetoka.

Zote hizo ni habari za uongo, ripoti ya daktari bado haijatoka na pia M2theP hajafariki dunia, ni mzima wa afya na amekua akiendelea vizuri.

Ameanza kufungua macho toka jana na hata kunyanyua miguu, kitu ambacho manesi wamesema ni matumaini kama akiendelea hivyo ndani ya siku tatu anaweza kuanza kuongea.


Baadhi ya Watanzania walikusanyika kupanga mipango ya kusafirisha mwili
Love to hear what you think!