Namnukuu akisema “ni kweli wamefanyiwa uhalifu hotelini kwao wakiwa hawapo, imeibwa Ipad pamoja na shilingi laki tisa, bado tunamtafuta mwizi ambae bado hajajulikana”
Juzi September 12 ndio askari anaetuhumiwa kusababisha kifo cha Mwangosi alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na baadae kurudishwa mahabusu.
Imekua ngumu kuwapata wahusika lakini mpekuziblog inaendelea kuwatafuta ili kujua mazingira ya wizi na kama kuna ushahidi wowote uliopotea pamoja na mambo mengine