Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.
SIKU chache baada ya kuahidi kumzalia mtoto mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Bushoke, mwigizaji wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amedaiwa kupata tatizo la mimba yake kuharibika.
Chanzo chetu makini kilitutonya kuwa, kuharibika kwa mimba hiyo kulibainika hivi karibuni huku mwenyewe akieleza kutojua sababu.
“Mwenyewe anadai hata hajui imeharibika kwa sababu gani lakini ukweli ndiyo huo, kwa sasa hana raha kabisa kwani alishaamua kuzaa lakini ndiyo hivyo tena,” kilidai chanzo hicho.
Katika kupata ukweli wa habari hiyo, mwandishi alimtafuta Jini Kabula na alipoulizwa juu ya mimba yake kuchoropoka alisema kwa masikitiko:
“Naomba unipigie baadaye nitakueleza kila kitu lakini ni ukweli kwamba ‘mwanangu’ ametoka.”