Mwanafunzi 
 aliyekuwa akisubiri kufanya  mtihani  wa kidato cha nne unaotaraji  
kuanza kesho Bw Khamis Mkundo mkazi  wa Mwangata C katika Manispaa  ya 
Iringa  akiwa amejinyonga  usiku  huu kuhofu  mtihani  wa kidato cha nne
 Mwenyekiti  wa serikali ya mtaa wa Mwangata C Bw Sarehe Mgimwa akisoma ujumbe  ulioachwa na marehemu huyu 
 Askari  kanzu  akikagua  mwili wa mwanafunzi  huyo  
 Wananchi  wa Mwangata  mjini Iringa  wakiwa nyumbani kwa marehemu  
 Mwili  wa kijana  huyo ukitolewa  tayari  kupelekwa  chumba  cha kuhifadhia maiti Hospital  ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa
| Mwili huo ukipakiwa katika gari la polisi | 
Mwanafunzi 
 wa  aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa 
akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne 
kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa 
Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba
 kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa 
kidato cha nne.
Katika  
barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  
hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara 
kwa mara  hiyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka na aibu katika mtihani ujao 
ambao anaamini angefeli.
Shemeji  
wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  huu   kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya  kati ya saa 
12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  
mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea 
kurisiti  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.
Kwani  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.
Hata  
hivyo kufuatia mazungumzo hayo kijana huyo aliangana na ndugu zake 
akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo 
kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.
Mwenyekiti 
 wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo 
 hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha .CHANZO MATUKIO 
DAIMA