Sunday, March 17, 2013

MWENYEKITI WA SIMBA ,ndg, RAGE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WANG'OLEWA


MKUTANO mkuu wa dharura wa wanachama wa klabu ya Simba umemwondoa madarakani mwenyekiti wao Ismail Rage na kuivunja kamati ya utendaji ya klabu hiyo kwa madai ya kukiuka katiba ya klabu yao.
Mkutano huo ambao kabla ya kufanyika kwake ulikuwa umepigwa marufuku na uongozi wa Simba kwa madai kwamba haukuwa halali ulifanyika kwenye Hoteli ya Starlight jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na  kuhudhuriwa na wanachama zaidi ya 600.
Mbali ya kumtimua Rage,mkutano huo pia ulimpendekeza  aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hans Pope na Rahma AL kharoos kuongoza kamati maalumu hadi pale uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapofanyika.
Mkutano huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mohamed Wandi na katibu wake Maulid Said ulikuwa na  agenda kuu moja iliyojadili mwendendo mbovu  wa klabu ya Simba kwenye Ligi Kuu inayoendelea na kutokuwa na imani  viongozi.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliokuwa na utulivu mkubwa huku ukilindwa na askari polisi wachache,Wandi alimlaumu  Rage kwa madai kwamba amekuwa akiiendesha  klabu yao pasipo kufuata katiba.
"Ibara ya 16 kipengele G inasema kutakuwa  na mkutano kila baada ya miezi minne kujadili maendeleo ya klabu lakini haujafanyika mpaka leo.
"Vilevile ibara ya 18 kipengele cha sita inasema kamati ya utendaji itaunda baraza la wazee na kifungu cha 28  C,kutakuwa na nafasi ya mwanamke katika kamati ya utendaji lakini imekiukwa,huku ni kusigina katiba,".alisema Wandi na kuongeza kuwa:
"Ibara ya 22 ya katiba ya  klabu ya Simba itupanawapata wanachama haki ya kuitisha mkutano endapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawatakuwapo na ibara ya 19 kifungu cha tatu inatupa mamlaka ya kumwandikisha na kumfukuza mwanachama,".
Baada ya kumaliza kusoma sehemu ya katiba ya klabu ya Simba aliyodai imekiukwa,Wandi aliwataka wanachama wenzake kuamua kama Rage na kamati yake ya utendaji ipewe muda zaidi au iondolewe ndipo wote waliponyoosha mikono juu wakitaka watimuliwe.





Love to hear what you think!