STAA wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amejikuta akiumbuka mbele ya mashabiki wake baada ya matiti a.k.a nido zake kuchomoza na kuonekana hadharani akiwa jukwaani na kusababisha midume yenye ukame kumzengea.
Tukio hilo la aibu isiyo na kipimo lilishuhudiwa na mwanahabari wetu usiku wa kuamkia Septemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambako kulikuwa na tamasha kubwa la Serengeti Fiesta 2012.
Baby Madaha alifanya kioja hicho baada ya kutakiwa kupanda jukwaani kuimba na Juma Kassim ‘Nature’ ambaye wameshirikiana katika moja ya nyimbo zake.
Bila hiyana, Baby alipanda stejini kwa mbwembwe na kujikuta akimwaga radhi kwa kuonesha matiti hadharani na kusababisha umati uliokuwa umefurika uwanjani hapo kulipuka kwa shangwe huku mwanadada huyo akiendeleza libeneke la shoo kali.
Baada ya kushuka jukwaani ndipo dada huyo alipovamiwa na wanaume wakware ambao walimbonyeza Kizenji hadi alipookolewa na mabaunsa na kupelekwa nyuma ya jukwaa.