WAZIRI Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, Jumamosi iliyopita alioa mwanamke mwingine katika sherehe ambayo haikufanyika kiserikali.
Tsvangirai (60) ambaye amemwoa Elizabeth Macheka (35), hakuweza kufunga ndoa kamili kiserikali kwa vile kuna mwanamke mmoja aliweka zuio la kufanyika kwa ndoa hiyo akidai waliwahi kuoana kimila.
Mke wa kwanza wa kiongozi huyo, aliyeitwa Suzan alifariki akiwa na umri wa miaka 50 katika ajali ya gari mwaka 2009.