Wednesday, September 11, 2013

Mwandishi wa gazeti la MWANANCHI akatwa katwa mapanga mkoani SINGIDA

Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa  mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. 

Awila ambaye amelazwa wodi 2   katika hospitali ya mkoa amedai kuwa  baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa  simu yake ya  kiganjani .

Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi
Love to hear what you think!