Friday, July 13, 2012

ALICHOKISEMA MAMA MZAZI WA KANUMBA KUHUSU HII KAMPUNI YA MAREHEMU KANUMBA.

Hiyo ndio ofisi ya Marehemu Steven Kanumba ambayo bado inaendelea na kazi kama kawaida Sinza Dar es salaam.
Exclusive on millardayo.com Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba amesema kampuni ya Kanumba The Great imeshaanza kazi tayari ikiwa chini ya usimamizi wa Abela au Mrs Bile ambae ni dada yake na Marehemu Steven Kanumba ambae Kanumba ndio alikua anamfata kwa kuzaliwa.
Mwingine alieteuliwa kuisimamia hiyo kampuni sasa hivi ni Seth Bosco ambae ndio anamfata Kanumba kwa kuzaliwa, ambapo sasa hivi kampuni itakua inarekodi movie na waigizaji mbalimbali chini ya uongozi wa Seth, haina mwigizaji pekee kama ilivyokua mwanzo, sasa hivi watatumika wasanii wote ambao itaonekana uwezo wao unaruhusu kucheza kwenye movie ambazo zinaandaliwa na kampuni hiyo.
.
.
Hii ni moja kati ya computer zilizotumika kuedit movie za Kanumba hapa kwenye ofisi yake Sinza.
Unaweza kulike au kutweet hii story ili na wenzako wa facebook na twitter waione, shukrani!


Love to hear what you think!