Wednesday, September 11, 2013

"Kwa sasa Sina MPENZI ....mwenye nia ya dhati ANITAFUTE"...Baby Madah

 
Leo katika interview na baby Madaha ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mnono na kampuni ya Candy n’ Candy Records  ya jijini Nairobi nchini Kenya , Bongomovie.com wameweza kupata mambo matano ambayo mashabiki wa mwanadada huyu watakuwa hawajui kumhusu yeye.
 
Katika interview hiyo, baby Madaha  ametaja mambo matano ambayo anasema mashabiki wake wanahitaji kuyafahamu kumhusu yeye. Mambo hayo ni haya yafuatayo:

1. I’m single ( Sina  mpenzi)
Mwanadada huyu amesema kuwa kwa sasa yupo single na  yuko  bize  na PESA. Ila  kama  kuna  mwanaume  mwenye  nia  ya  dhati  anaweza  kumtafuta.

2. Anasoma degree ya sanaa kwenye sayansi ya siasa na historia (B.A- Political science and History) - chuo kikuu huria jijini Dar es Salaam..

3. Mama yake mzazi ndio rafiki yake mkubwa maishani

4. Ni mpenzi wa soka na ni mshabiki wa Chelsea na anavutiwa na  Kevin-Prince Boateng wa club Schalke 04 ambaye ndiye alisababisha akanyoa nywele staili aliyonayo baby madaha kwa sasa.Love to hear what you think!