Sunday, June 23, 2013

TASWIRA ZA KILI MUSIC TOUR NDANI YA DODOMA

Hatimaye ile ziara ya Muziki Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imeanza rasmi leo kwa show baab kubwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Katika onyesho hilo lililohusisha wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012 kwa utangulizi wa waendeshaji wake Dulla na Zembwela kutoka East Africa TV kugawa zawadi kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa kuendesha mashindano mbali mbali.
Hakuna ubishi kuwa Ben Pol ndiye mfalme wa R&B na alilithibitisha hilo alipoponda jukwaani na kuwaimbisha…
Hatimaye ile ziara ya Muziki Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imeanza rasmi leo kwa show baab kubwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma. Katika onyesho hilo lililohusisha wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012 kwa utangulizi wa waendeshaji wake Dulla na Zembwela kutoka East Africa TV kugawa zawadi kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa kuendesha mashindano mbali mbali.
Hakuna ubishi kuwa Ben Pol ndiye mfalme wa R&B na alilithibitisha hilo alipoponda jukwaani na kuwaimbisha mashabiki wake mwanzo hadi mwisho kwa nyimbo zake kali Pete, Jikubali, Samboira huku kivutio kikiwa pale uwanja mzima ulipoimba pamoja nae wimbo wa Nikikupata.
Malkia wa Bongo Flava, Lady Jaydee ambaye ni mwanamke pekee katika wasanii waliokuja Dodoma alithibitisha kwamba habahatishi baada ya kulishambulia jukwaa kwa nyimbo zake zote zililizompa umaarufu. Jide nae kama wasanii wengine alianza kwa kumkumbuka marehemu Albert Mangwea kwa kuimba chorus ya wimbo wa "Sikiliza" ambao ni ushirikiano wake, MwanaFalsafa na Mangwair kisha kuanza kuimba nyimbo zake kali na kumalizia na Joto Hasira alioshirikiana na Profesa Jay aliepanda jukwaani kuungana nae.
Profesa Jay anapenda kuitwa The Heavy Weight MC na alililithibitisha hilo wakati alipokabidhiwa jukumu la kufunga show, kwa zaidi ya nusu "Jay wa Mitulinga" kama anavyojulikana aliwaimbisha mashabiki nyimbo zake kali toka Bongo Dar es Salaam, Chemsha Bongo, Piga Makofi nk. Kivutio kilikuwa pale alipoimba wimbo wake wa zari la mentali na kumpandisha jukwaani moja ya mashabiki kuimba mistari ya "Zubeda" huku akishangiliwa na wengi kabla ya kuendelea kuchana nyimbo zake nyingine zilizompatia umaarufu.
Alipotajwa kuwa zamu yake imefika ulitokea mtafaruku wa mashabiki kusukumana kila mmoja akitaka kuwa mbele ili amuone vizuri, lakini huyu ndiye Mfalme wa Hip Hop kwa mwaka 2012, Kala Jeremiah ambaye alilishambulia jukwaa kwa zaidi ya nusu saa huku akwadatisha maelfu waliojitokeza huku kama kawaida wimbo wake wa Dear God ukionekana kumgusa kila mtu.
Wa kwanza kupanda kwenye steji alikuwa Linex "Mjeda" alieimba nyimbo zake zilizotamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni. Wimbo ulioonekana kuwakonga wengi ulikuwa "Aifola".
Wa pili jukwaani alikuwa ni Ommy Dimpoz aliepanda jukwaani na madansa wake wanaosifika kwa uhodari wao wa kumiliki jukwaa na kuimba nyimbo zake mbili za Baadae na Me and You kabla ya kushuka na kumpisha Ben Pol.
Roma! Roma! Roma! ndio kelele zilizopigwa na mashabiki wakati akipanda jukwaani na kama ilivyo kawaida ilikuwa ni michano mwanzo hadi mwisho. Roma ambaye mwaka jana alishinda tuzo mbili alizidi kuonyesha ubora wake pale alipoimba nyimbo zake kama "Pastor", "Tanzania", "Kidole cha mwisho juu" na "2030" huku akitumia dakika kadhaa kumkumbuka marehemu Albert Mangwair.
---
Show hiyo iliisha mnamo saa nne huku ikiwa imekidhi kiu ya mashabiki wengi wa burudani wa Mkoa wa Dodoma na inatarajia kuendelea mkoani Tanga Jumamosi wiki Ijayo.Love to hear what you think!