Thursday, October 3, 2013

KAMA HUKUIPATA HII ANGALI PICHA ZA VURUGU ZA MBAGALA LEO


Askari kanzu katika jitihada za kuwatawanya waandamanaji.
Mojawapo ya matairi yaliyochomwa na wananchi.…
Askari kanzu katika jitihada za kuwatawanya waandamanaji.
Mojawapo ya matairi yaliyochomwa na wananchi.
Waananchi wakiandamana wakati wa vurugu hizo.
Askari polisi wakiwa eneo la tukio.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Temeke, Engelbert Kiondo (wa tatu kulia) akiwa katika eneo la tukio.
Kamanda Engelbert Kiondo (wa pili kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kizuiani, Mashaka Selemani (wa kwanza kushoto).
Kamanda Kiondo akitoa maelekezo kwa baadhi ya askari wake.
Wananchi wakiwa eneo alipogongwa mwanafunzi.
Kikosi cha polisi jamii kikiwa eneo hilo.OCD wa Mbagala, Jonathan Shanna akiwasiliana na kikosi chake.
LEO asubuhi majira ya saa nne na nusu kumetokea vurugu kali za wananchi eneo la Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam.
Vurugu hizo zilitokea baada ya mwanafunzi mmoja kupoteza maisha kwa kugongwa na lori lenye namba za usajili  T 632 BVY. Baada ya ajali hiyo, wananchi walifunga barabara kwa mawe na kuchoma matairi wakizuia magari kupita katika barabara ya Kilwa jambo lililopelekea polisi kuingilia kati. Ili kutuliza vurugu hizo kutoka kwa wananchi waliokuwa wanadai kuchoshwa na ajali zinazotokea mara kwa mara eneo hilo, polidi walilazimika kutumia mabomu ya machozi pamoja na kupiga risasi hewani katika kuwatawanya wananchi.
(Picha na Makongoro Oging’ / GLP)




Love to hear what you think!