Monday, April 22, 2013

Mahakama ya rufaa yatupilia mbali Rufaa ya Kupinga ushindi dhidi ya Lema!!Ombi la kwanza la waleta rufani la kutaka review ya uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa juu ya kesi ya Mh.Lema na kutaka isikilizwe na jopo la majaji 7 limetupiliwa mbali leo katika mahakama ya rufaa na sasa ni majaji walewale waliotoa hukumu wanapitia.Mahakama imetupilia mbali madai ya kwanza kwa kuwa hayapo based on merits


Kesi hii ilifunguliwa tena baada ya Mh.Lema kushinda rufaa tarehe 21 desemba 2012,kesi iliyosimamiwa na mawakili maarufu sana baada ya kuzungushwa kwa muda mrefu.Warufani safari hii wanataka mahakama ipitie upya uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu na wametaka benchi la majaji saba.


Mahakama imetupilia mbali mashtaka yao na mahakama imewaamuru tena wakata rufaa walipe gharama zote za kesi.

Wafuasi wa CHADEMA wanashangilia sana muda huu eneo la mahakamaLove to hear what you think!