Monday, April 22, 2013

Wakenya Wasema "Mr.Nice anafaa kuheshimiwa, anakipaji special ambacho kinafaa kutunzwa"

Siku chache baada ya record lebel ya Grand Pa ya Kenya kutangaza kumsaini Mr. Nice, DNA ambae pia ni member wa lebel hiyo amefunguka kuhusu jinsi walivyompokea member huyo mpya katika familia ya Grand Pa.

Akizungumza na Milazo 101 ya Radio One amesema Mr. Nice anafaa kuheshimiwa kutokana na uwezo wake na kwamba ana kipaji special ambacho kinafaa kutunzwa. Amefafanua kuwa wao ndio waliomtafuta mwanamuziki huyo ambae wanaamini bado anapendwa sana na fans wake hususani nchini Kenya.

“Mr. Nice hakuomba nafasi tulimtafuta sisi, kwa sababu tunatambua kipaji chake na tunajua kwamba wasanii sio kama karatasi ya choo, sio kama mtu akinyamaza amepotea na tena hana kazi. May be unakuta labda hako na management ama kuna issue flani ya kibinafsi mtu akanyamaza. Mr. Nice ndiyo kabisa kutoka Tanzania ianze yeye ndiye alifanya bongo ikajulikana Afrika mashariki na anafaa apewe nafasi tena na tena na tena.”

Alifunguka zaidi kuwa Grand Pa kwa kushirikiana na Mr. Nice wanaweza kumrudisha Yule Mr. Nice wa kipindi kile.

“Grand Pa kwa kushirikiana na Nice anaweza akarudi, Grand Pa yenyewe haiwezi. Nice mwenyewe alifanya nyimbo ambazo sasa hivi bado zinagongwa Kenya baada ya miaka nane miaka kumi unajua, it means jamaa bado ako na kipaji special ambacho kinafaa kutunzwa. Wasanii wengi wanavipaji lakini wanakosa kufaulu because hawana Management, ndo hivyo sasa Mr. Nice yuko ndani ya Nyumba tunafanya nae.”

Hata hivyo uongozi wa Grand Pa umemzuia kwa muda Mr. Nice kuzungumza na Media kwa sababu za kiutawala hadi pale watakapoanza tour yake nchini Kenya hivi karibuni.


Love to hear what you think!