Friday, February 15, 2013

JOHARI MJAMZITO


LEJENDARI katika tasnia ya sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ anadaiwa kuwa kitumbo ndii, ishu ambayo imeibua maswali tata kwa watu wake wa karibu huku mwenyewe akichekelea.
Kwa mujibu wa chanzo makini cha habari hii,
kwa sasa mwanadashosti huyo ana dalili zote za kuwa na kibendi lakini mwenyewe anafanya siri.
Baada ya kuzinyaka habari hizo zinazoendelea kushika kasi mitandaoni,  wanahabari wetu walifunga safari hadi ofisini kwa Johari, RJ Production,
Sinza-Mori, jijini Dar lakini hakupatikana ndipo akapigiwa simu ambapo mahojiano yalikuwa hivi;Mwandishi: Haloo Johari, mambo vipi?
Johari: Poa tu, sijui naongea na nani?
Mwandishi: Unaongea na waandishi wa gazeti la Ijumaa, tumefika ofisini kwako haupo, kuna habari kuwa wewe ni mjamzito. Je, ni kweli?
Johari:  (anacheka sana) Mh! (kicheko tena na tena) Hahahaaa (kicheko tupu)...niko location (mandhari ya kurekodia filamu), nani amekwambia mimi ni mjamzito?
Mwandishi: Mtu wako wa karibu. Kwani huo ujauzito una muda gani na baba mtoto wako ni nani?
Johari: Jamani watu wabaya, hivi nyiye  mnamjua baba yake?
Mwandishi: Hatumjui ndiyo maana tunauliza.
Johari: Jamani kwani nikizaa kuna ubaya gani? Hata hivyo, kuzaa ni jambo la heri, nitakupigia baadaye.
Hata hivyo, hadi habari hili inakwenda mtamboni Johari hakupiga kama alivyoahidi.Love to hear what you think!