Thursday, November 29, 2012

MUUMINI WA KIISLAMU (SHOGA) NCHINI UFARANSA AJIANDAA KUANZISHA MSIKITI MAALUMU WA MASHOGA WA DINI IYO

Ludovic Mohammed Zahed





Ni wazi kabisa, hili halitawapa faraja waamini wa Uislamu kote duniani, na kwa jinsi ambavyo tumeona migogoro ya kiimani ikiendelea kuigubika dunia siku za karibuni, hili la sasa huenda likafanya migogoro hii ikawa ndio mwanzo wa vita ya tatu ya dunia. Kama huamini, sikia habari hii
Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia, muumini mmoja wa dini ya kiislamu huko nchini Ufaransa, anajiandaa kuanzisha msikiti ambao utakuwa ni mahususi kwa ajili ya waumini wa dini hiyo walio mashoga.
Ludovic Mohammed Zahed, amejiweka tayari kabisa kwa ajili ya kukabiliana sio tu na changamoto atakazokumbana nazo kwa uamuzi wake huo, bali pia kwa mabaya mengine yoyote yatayojitokeza huku akijua kuwa mambo hayo ambayo anajiandaa kuyakabili, lazima yatamtokea. Zahed, sio tu kwamba ni muumini wa kiislamu, bali pia ni mchambuzi aliyebobea katika imani hiyo na anajiandaa kuanzisha msikiti huo katika mji wa Paris, mwishoni mwa mwezi huu.
Tunahitaji kuwa na sehemu ya usalama kwa ajili ya watu ambao wanajihisi hawako salama na huru sana pindi wanapokuwa katika misikiti ya kawaida. Wapo wanawake hawapendi kuvalia vitambaa hadi usoni au kukaa nyuma wawapo misikitini, wapo wanaume ambao hawana hisia za kiume na wanajihisi wanapokuwa mbele za watu hawajisikii uzuri, na mradi huu sasa ni kwa ajili ya kuwaletea matumaini mapya katika kuabudu.



Love to hear what you think!