Wednesday, April 17, 2013

WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa baada Gari aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana Usiku. Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya

Gari aina ya scania yenye nambali za usajiri T578 ALS likiwa na tela nambli T125 AGM lililobomoa nyumba na kusababisha vifo vya watu 3 wa familia moja

Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi hii ni miili ya watu walifariki kwa gugongwa na roli hilo

Wananchi wa kijiji cha Ilongo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wakiwa msibani
WATU watatu wamefariki dunia na wengine wawili wa familia moja kujeruhiwa baada Gari aina ya Scania kuvamia Nyumba yao wakiwa ndani jana  Usiku. Ilongo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
  
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa Tatu na Robo usiku katika Kijiji cha Ilongo Wilaya ya Mbarali Mkoani hapa.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa ajali hiyo ilihusisha  magari kugongana na kugonga nyumba na kusababisha vifo na majeruhi.


Alisema chanzo cha ajali kilitokana na Gari lenye namba za usajili T578 ALS likiwa na tela lenye namba za usajili T125 AGM aina ya Scania likiendeshwa na dereva ambaye hakuweza kutambulika liligonga  kwa nyuma  gari lenye namba T959 ASC aina ya Scania.
  
Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Juhudi Saimon(34)Mnyiha mkazi wa Dar Es Salaam kisha gari hilo  kugonga nyumba mali ya Matia  Mwagala mkazi wa Kijiji cha Ilongo.
  
Aliwataja matrehemu kuwa ni Asia Yahaya (52)mkulima na Msangu, Abubakari Yahaya(8) Msangu na mwanafunzi darasa la pili  aliyekuwa anasoma katika Shule ya msingi Ilongo na Fatuma Yahaya (6) Msangu mwanafunzi wa darasa la kwanza  Shule ya Msingi Ilongo wote wakazi wa kijiji hicho.

Aidha aliwataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni pamoja na Abuu  Fadhil (22)Mzigua mkazi wa Dar Es Salaam ambaye ni tingo wa gari lililogonga Nyumba pamoja na Steven  Chiwa (26) mbembe raia na mkazi wa Nchi jirani ya Zambia ambaye ni msindikizaji wa gari hilo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Misheni ya Chimala.
  
Hata hivyo wa dereva wa gari lililosababisha ajali alikimbia na gari mara baada ya tukio ambapo Kaimu Kamanda  anatoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu ya mahalialipo dereva wa gari lililosababisha ajali hiyo azitoe katika mamlaka husika ili akamatwe na sheria ichukue mkondo wake, vinginevyo ajisalimishe mara moja.
  
Wakati huo huo  Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia  Asajile Mwamtina (46) mkazi wa kijiji cha Syukula Wilaya ya Rungwe mkoani hapa akituhumiwa kufanya mapenzi na binti yake wa miaka 13.
  
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa lilitokea juzi  majira ya saa Kumi na Mbili jioni baada ya kumvizia binti huyo (jina limehifadhiwa) ambaye aliacha shule akiwa darasa la tano mwaka 2011 kwa matatizo ya ugonjwa wa kifafa akiwa anapika.
  
Alisema mtuhumiwa alipata mwanya wa kufanya unyama huo kutokana na mkewe  ambaye  mama mzazi   wa mhanga huyo Tumikigwe Samalinga akiwa kijiji cha Kiwira kuuguza mgonjwa na kuongeza kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika.
  
Aidha katika tukio lingine eneo la Makunguru Jijini Mbeya Vyumba 12 vya biasharaa viliteketea kwa moto jana majira ya saa Tano asubuhi vilivyokuwa vimetoka kujengwa  mali ya Dominick Mbinga Mkazi wa Dar Es Salaam.


Hata hivyo hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza baada ya moto huo kudhibitiwa kwa ushirikiano baina ya kikosi cha zima moto na uokoaji na wananchi.


Thamani halisi ya uhalibifu bado kujulikana pamoja na chanzo ingawa kwa mujibu wa majirani walisema inawezekana ikawa ni hitilafu ya umeme kutokana na muda huo wapangaji wa nyumba hiyo kutokuwepo wakati moto ukitokea ambao ulijulikana baada ya majirani kuona.Love to hear what you think!