Friday, November 30, 2012

HIVI NDIVYO BLACKBERRY ILIVYOSAIDIA KUWANASA WALIOIBA KWENYE AJALI YA SHARO MILIONEA

SIMU aina ya Blackberry ndio chanzo cha kuwanasa wezi pamoja na baadhi ya vitu vilivyoporwa  katika ajali ya msanii wa filamu na muziki nchini, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, mapema leo alithibitisha kupatikana vitu hivyo, baada ya msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali wilayani Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi.
Saluti5 ilimnukuu kamanda huyo akisema: " Jeshi la Polisi liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya ‘blackberry’ ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza.
"Wakati walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo" alifichua Kamanda huyo.
Alivitaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, betri ya gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka mara baada ya kutokea ajali hiyo.Chanzo:www.saluti5.com



Love to hear what you think!