Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Mwangata mjini Iringa baada ya uvumi kuwa kuna msukule kaonekana eneo hilo.
Polisi wakidumisha amani na kuwasaka walioeneza uvumi huo.…
Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Mwangata mjini Iringa baada ya uvumi kuwa kuna msukule kaonekana eneo hilo.
Polisi wakidumisha amani na kuwasaka walioeneza uvumi huo.
Shughuli zikiwa zimesimama baada ya taarifa hizo za kuwepo msukule.
ZIMEZUKA habari zenye utata ambazo hazijathibitishwa mkoani Iringa
kuwa mtoto mmoja anayedaiwa kufa na kuzikwa kuonekana leo akidaiwa
kuwekwa Msukule.
Tukio hilo limetokea eneo la Mwangata mjini
Iringa na kupelekea polisi kufika kuwatawanya wananchi
waliokusanyika eneo hilo na kuwasaka wale wanadaiwa kueneza uvumi huo.
Hata
hivyo hakuna mwananchi hata mmoja kati ya waliokuwepo eneo hilo ambaye
amethibitisha kuona msukule huyo zaidi ya kila mmoja kusema amesikia.
Wananchi hao wameizunguka moja kati ya nyumba eneo hilo wakitaka kuichoma moto kwa madai kuwa ndani kuna msukule huyo.
Habari / Picha kwa hisani ya : FRANCIS GODWIN BLOg