KWELI KIGOMA ALL STARS WANAHITAJI PONGEZI!
- 'Una la kuongeza'
- Kigoma all stars!
- Zitto akisisitiza jambo
- Zitto Kabwe alipokutana na Kigoma All Stars
- Zitto, Queen Darlin, Mwasiti na wengine
-
- Huu
ni mwaka ambao mkoa wa Kigoma utaongelewa sana kwenye burudani.
Hongera nyingi ziende kwa yule aliyekuja na wazo hili lenye thamani
ambalo limeunyanyua mkoa wa Kigoma katika kipindi kifupi mno.
- Tangu itoke
Leka Dutigite, Kigoma imejipatia sifa kubwa kwa kujulikana miongoni
mwa wasanii waliojuu kwenye muziki wa kizazi kipya nchini kuwa
wanatokea huko.
Ukizungumzia Diamond Platnumz na ukaona jinsi kijana alivyofanikiwa
mpaka kupiga show Big Brother, ni halali uheshimu mkoa ulio asili yake,
Kigoma. Tunafahamu kimaendeleo Kigoma ni miongoni mwa mikoa iliyonyuma
kwa Tanzania. Wanapaita ‘Kigoma mwisho wa reli’. Jitihada hizi za
mbunge wa Kigoma kaskazini, Mheshima Zitto Kabwe kuwapa support wasanii
wenye asili ya Kigoma, sasa zimegeuka mfano wa kuigwa.
Tangu wimbo ‘Leka Dutigite’, neno la kiha lenye maana ya Acha Tujidai,
Kigoma umekuwa ni mkoa unaojadiliwa sana na wapenzi wa burudani mitaani
na kwenye mitandao ya kijamii. Na hapo ndo utakapogundua kuwa Tanzania
hakuna ukabila. Watu wa mikoa mingine wameupenda wimbo huu na
kuwapongeza wasanii hao.
Ni wimbo uliofanywa na masupastaa haswaa wa Tanzania. Diamond, Peter
Msechu,Ommy Dimpoz, Baba Levo, Banana Zorro, Chege, Mwasiti, Linex,
Queen Darling, Rachel na wengine wasanii waliojuu sana nchini. Ni
movement ambayo ikiwa nyuma ya mbunge mwenye kipaji cha uongozi, Mhe.
Zitto, inayoweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mkoa huo, kiuchumi na
kisiasa.
Ni muungano unaoweza kupeleka maendeleo makubwa kwa kutumia mwavuli wa
burudani. Ni movement ambayo itawaamsha wasanii wengine na hata watu wa
kawaida kuthamini asili yao. Wanasema mtu asiyekuwa na kwao ni sawa na
mtumwa. Itawaamsha wasanii waliopo Dar es Salaamn(kitovu cha tasnia ya
burudani nchini) kujivunia mkoa ama hata kijiji anachotokea. Chema
vizuri kuigwa.
Mikoa mingine haitakuwa na hasara ikifanya hivyo pia. Uzuri wa muungano
kama huu, huchangia kukua kwa sanaa kwenye mkoa husika. Tangu Leka
Dutigite itoke, kuna wasanii wengi wachanga wa mkoani Kigoma waliopata
morali ya kuongeza juhudi zaidi kimuziki ili wafanikiwe na hatimaye
kupewa heshima kama hiyo ya kujiunga na wakali wa mkoa huo. Japo baadhi
yao kama wanavyosema kuwa Kigoma ni asili yao tu lakini hawakukulia
huko, asili ipo pale pale na ni jambo la msingi kuutangaza.
Baada ya kitendo hicho, leo hii watu wengi wametamani wasanii wa mikoa
yao wafanye kitu kama hicho pia. Huo ni wivu wa maendeleo kama asemavyo
Monty Khatau Ezel, “Nimevutiwa na hiyo kitu, natamani ningekuwa
natokea Kigoma,nina ugonjwa wa wivu wa maendeleo,najivunia kutokea
kusini,LINDI wajiandae mafanikio yanawajia.”
Ibrahim Athumani Masokola naye anasema, “Nahisi katika mambo ya kuiga
kwa baadhi ya watu kama waheshimiwa ni pamoja na hili analofanya mhe
Zitto kwani ni njia mojawapo ya kuwafikia wananchi kwa urahisi HONGERENI
SANA WOTE mlohusika kwa namna moja au nyingine.”
Naye Zulu Agrey Mnkeni anasema, “Natamani nami ningekuwa wa KIGOMA ila
ndo bahati mbaya natoka KILIMANJARO naogopa kuitwa MKABILA.”
Kitendo hicho cha Mheshimiwa Zitto kuungana na wasanii ili kuutangaza
mkoa wa Kigoma,kinamweka karibu zaidi na vijana waliowengi nchini na
kumsafishia njia yake kwa mambo makubwa zaidi katika career yake kama
mwanasiasa. Hongereni Kigoma All Stars!