Saturday, January 3, 2015

SIKUKUU YA MAULID KITAIFA KUFANYIKA KOROGWE, TANGA-BAKWATA


Sikukuu ya Maulid kitaifa inaratajia kufanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga Januari 4 Mwaka huu.
Kwa taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Tanzania (Bakwata),Suleiman Said Lolila ilisema Maulid itaanza Januari 3 na kumalizika Januari 4.
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania ,Issa  Bin Shaaban Simba anawatakia waislaam na wananchi kwa ujumla maulid njema.
Hata hiyo Katibu Mkuu Lolila aliwataka waislam wote nchini kushirikia kikamilifu katika mazazi ya M.tume mohamad (S. AW)

Wabillah Tawfiq.Love to hear what you think!