Monday, June 16, 2014

KIJANA AKUTWA AMEKUFA KWENYE KITUO CHA MABASI YAENDAYO KASI DAR


...kama vile kalala kumbe ndiyo kafa.Mmoja wa mashuhuda wa tukio.Mtendaji wa eneo hilo na baadhi ya Wasamaria wakiufunika mwili wa marehemu.Mtendaji wa kata ya Midizini-Manzese Bw. Penford Kizo akiwa mahali pa tukio.
KIJANA mmoja wa kiume aliyedaiwa kuwa ni mfanyabiashara ndogondogo amekutwa amefariki katika kituo cha mabasi yaendayo kasi Manzese, jijini Dar, leo asubuhi.  Inasemekana vijana wengi huwa wana tabia ya kulala ndani ya vituo hivyo kwa hiyo watu iliwachukua muda mrefu kubaini kama amefariki.
Kwa mujibu wa mtendaji wa serikali wa Kata ya Midizini-Manzese, Penford Kizo na mashuhuda wengine, kifo cha kijana huyo hakijafahamika kimesababishwa na nini.
(Picha / Habari: Gabriel Ng’osha na Mussa Mateja / GPL)



Love to hear what you think!