Monday, July 9, 2012

SHIGONGO KUTAPELIWA NA WALIOJIDAI MAMENEJA WA MSANII CHAMELEONE TOKA UG

Msanii Chameleone akiwa Airport, panaposemekana alizuiliwa kuondoka kwa kunyang'anywa Passport na Shigongo


Chameleone binafsi anasema balaa hilo limetokea jana wakati anajiandaa kuondoka nchini mida ya saa nane kasoro ambapo mmoja wa wafanyakazi wa Shigongo alimuomba passport yake na za wenzake wawili aliokuja nao ili watoe photocopy baada ya hapo akaambiwa kuwa Shigongo amechukua passport zao ili alipwe hela aliyotapeliwa mwanzo kiasi cha dola 3500 ambazo alitoa kama deposit ya msanii huyo kuperfom.


Chameleone aliendelea kudai kuwa kwa upande wake hahusiki na utapeli huo kwani watu ambao anamhusisha nao amewasikia kupitia kwa msanii wa kirundi Kidum ambaye ndiye aliyemconnect na watu hao, Chameleone alisema ‘mimi nilishangaa Kidumu aliponipigia simu na kuniuliza kama nakuja tz, nikamuuliza mbona sijui kitu? akasema sii hela umepewa kupitia meneja wako, nikamwambia meneja wangu hajapokea pesa yeyoye! Sasa nilivyofuatilia nikagundua watu ambao walimtapeli walimwalika Shigongo Kampala na kumwambia kuwa ni managers wangu na kitu walichofanya ni kutumia gari kama langu aina ya range rover nyeupe ambayo mimi natumia bila number plate wakamwambia kwamba wanahusika na mimi ndio maana ametuachia gari lake. Kuona hivyo Shigongo akatoa deposit nusu ya pesa ya shoo ambayo ilikuwa iwe dola elfu 7 baada ya hapo jamaa wakakata mawasiliano sasa Shigongo ananihusisha vipi na watu ambao mimi siwajui amwambie Kidum arudishe kwa sababu yeye ndiye aliyempa contact ya huyo meneja feki’.


Love to hear what you think!