Thursday, September 12, 2013

Selaa Stei Faa na Wife Wa Bosi

INAKUWAJE watu wangu wa nguvu? Ama nini? Kitaani hapa ni mpango mzima pipo wanakula tu wepesi. Kitaa hiyo kwa wanyama wangu inakuwa nini? Basi mia!
Sam taimu ukicheki laifu linavyomuvu utagundua kuwa halitaki mizinguo kabisa wanangu. Usawa umekaba kinoma aisee.
Tudei tusikie komfesheni ya mwanangu Kondo wa hapo Mabibo. Msela ana bonge la kisa. Yaani…yaani hata mi Mpeke nimesanda na kujikuta mwili ukinisisimka.
Msela Kondo alitimba tauni Dar miaka kadhaa iliyopita. Alipofika tauni kitaa cha Mabibo laifu halikwenda freshi hata kidogo kozi ndo alikuwa amemaliza standadi seveni so dili zikawa za kumulika na tochi.
Wani dei selaa aliamua kwenda kuomba jobu katika kampuni moko la usafirishaji lenye skani lake hapo kitaa cha washua Masaki.
Jombaa alipotimba aliambiwa ishu kama hizo akamuone mkurugenzi kitambi meneja au bosi kubwa wa kampuni.
Jembe anakuteli kuwa alipozama kwa ofisi akamsomesha mtu mkubwa ili apate jobu? Kilichozingua ni shule kichwani kwani mwana alipoulizwa kama yupo fiti klasi ikawa mtihani.
Mwanangu alipomwambia mkubwa kuwa kaishia standadi seveni, meneja akamfungukia kuwa hawezi kupata jobu kozi skonga hamna kichwani.
Basi msela akatolewa nishai pale mbele ya totozi wakare ofisini bati alipokompleini kwa sana akaambiwa aibuke neksti wiki.
Afta wani wiki msela akatimba. Bahati nzuri msela akaambiwa kuwa awe anasaidia kumuvuzisha na kufuta mafaili huku akitakiwa kuwa smati katika engo hiyo.
Unaambiwa mnyama mwenyewe alimshukuru bigi bosi theni akazama mzigoni na watoto wazuri. Hapo ndo problemu ilipoanzia.
Msela akawa amewaelewa wale watoto wazuri. Mwanzoni alizuga kuwa mgumu kwa mashori bati baadaye akalainika.
Kilichowafanya wale watoto pale jobu kumshobokea mwana ni kwa sababu alikuwa hendisamu wa ukweli kabisa.
Siku moko taimu ya kuondoka jobu kwenda maisha plasi ilifika bati mmoja wa wale mashori alimtonya kachaa kuwa kuna kazi ya kusaka mafaili f’lani so chalii ikabidi amsubiri. Kumbuka yule mtoto mzuri naye alikuwa waifu wa mtu na pia alikuwa ni kabosi kadogo pale jobu kozi ukitoka kwa meneja yeye ni kama mtu wa nne hivi so naye alikuwa na saundi.
Kweli jamaa aliminya huku akitafuta mafaili hadi giza likazama. Alipouliza vipi, chaliiangu akaambiwa asijali atapelekwa homu kwake na kupewa mshiko wa muda wa ziada.
Huku na huku mwana akasapraizi kumuona yule bimdashi anaklozi mlango na kuanza kumchezea maeneo hatarishi ya bodi lake jamaa akaona isiwe kwere.
Ishu za kutafuta mafaili tupa kule…kilichofuata stori ikawa fulu mchelemchele.
Kesho yake acha shosti asimulie jinsi alivyopigishwa kwata na jembe langu. Si totozi nyingine pale jobu nazo zikataka mambo? Ikawa ni dozi mtindo mmoko hadi akashtukiwa na bosi kubwa.
Alichokifanya meneja ni kumkolu kachaa na kumuonya kozi mmoja wa wale mashori alikuwa ni kifaa cha meneja. Chezea bosi kubwa wewe?
Mwana akajifanya kichwa ngumu. Akajisahau akawa anaendelea kukaribia meza wakati hachangii anachomeza! Unapenda mteremko? Basi umeuawa.
Baada ya bosi kubwa kuona jamaa anaendelea kufaidi vinono si ndo akawekewa mtego? Kudadeki! Cha mtu ni poisoni aisee. Aliponasa kabang…ndo akajikuta akirukwa ukuta, jobu ikaisha hapohapo na sasa anasikilizia maumivi kitaani. Wana mpo? Stei faa na waifu za mabosi kubwa la sivyo utaumbuka!
Love to hear what you think!