Thursday, September 19, 2013

MZEE MAJUTO AITWA BAKWATA


Stori: Imelda Mtema
SIKU chache baada ya ndoa ya supastaa wa vichekesho Bongo, Amir Athuman ‘Mzee Majuto’ kuvunjika, mke aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) kutoa malalamiko yake, Amani liko mbele kukuhabarisha.
Cheti cha ndoa.
Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee Majuto, Septemba 14, 2013 alikimbilia Makao Makuu ya Bakwata Wilaya ya Kinondoni yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msichana huyo, mambo aliyoyazungumza kwenye ofisi hiyo ni matatu, kwanza kutopewa talaka baada ya kuachika.
Akasema akimuuliza Mzee Majuto kuhusu talaka yake anamwambia amempa mwanamke mmoja aitwaye Rehema amfikishie, akahoji:  “Kwani huyo Rehema ndiye aliyenioa?”
Rehema Omar na mumewe Mzee Majuto siku ya ndoa yao.
Pili, akasema wakati anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo alimwachisha kazi mahali na pia alimhamisha kwenye chumba alichopanga.
Tatu, akasema kutokana na hayo yote anaomba alipwe fidia ya fedha kwa sababu ya usumbufu alioupata.
Rehema akasema kutokana na malalamiko yake, viongozi wa Bakwata walimpa barua ya kumfikishia Mzee Majuto yenye kichwa cha habari cha WITO.
Rehema Omar.
Mzee Majuto anatakiwa kufika bila kukosa kwenye ofisi hizo, Septemba 23, mwaka huu ambayo itakuwa Jumatatu ili shauri lake na mwanamke huyo lizungumzwe.
Juzi, Amani lilimpigia simu Mzee Majuto lakini muda wote iliita bila kupokelewa.
Toleo la gazeti hili lililopita, tuliandika ukurasa wa mbele habari yenye kichwa; NDOA YA MZEE MAJUTO YAVUNJIKA. Kwenye utetezi wake, mzee huyo alisema alimwacha mwanamke huyo baada ya kugundua hajatulia.
 
Mzee Majuto.Love to hear what you think!