Sunday, September 15, 2013

"Erick Shigongo ameamua kunichafua magazetini kwa kuwa nina kesi nae mahakamani"...Irene Uwoya.

 
Irene Uwoya amejibu mapigo ya kudaiwa kuiba simu aina ya iphone 5 toleo jipya la  mwaka  huu ambapo habari hiyo iliripotiwa jana  katika gazeti la Risasi na kutawala mitandao mingi  ya  kijamii. 

Katika  utetezi  wake  alioutoa  kupitia  ukurasa  wake  instagram, Irene  Uwoya amesema kuwa chanzo cha kuandikwa hivyo ni kuvunjwa nguvu katika harakati zake za kesi aliyomfungulia Shigongo

HII  NDO  KAULI  YAKE  :

 "Mi ni mti wenye matunda milele siogopi kupigwa mawe…
 
"Shigongo kaamua kunichafua coz nina kesi nae mahakamani…anadhani nitaiacha never yeye aponde anavyoweza ila mwisho wa siku sheria itafuata mkondo wake….

"Mi na yake mengi nayajua ila ngoja ninyamaze nisimwagiwe tindikali"Love to hear what you think!