Saturday, September 14, 2013

MTUHUMIWA UBAKAJI AHENYESHA POLISI

Na Abdi Suleiman, Zanzibar
KATIKA hali isiyo ya kawaida, kijana Faizi Haji Juma (22), mkazi wa Mchanga wa Kwale Wilaya ya Chakechake, Pemba aliwashangaza wananchi baada ya kuwatoroka askari waliokuwa wamemdhibiti ndani ya jengo la mahakama ya wilaya hiyo.
Kijana huyo anayekabiliwa na makosa mawili katika mahakama mbili tofauti, likiwemo la ubakaji na shambulio la mwili kwa lengo la kutaka kubaka, aliwachomoka askari na kukimbilia baharini katika Soko la Katari.
Baada ya kukimbia kwa muda, askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Agustino Awe na Koplo Mohamed Hamza, walilazimika kumkimbiza kwenye matope na kuhakikisha wanamtia mikononi mtuhumiwa huyo na kumrudisha mahakamani.
Baada ya kurudishwa ndani ya viunga vya mahakama ya wilaya, mtuhumiwa huyo alitakiwa kuieleza korti sababu zilizomfanya akimbie lakini akaishia kubabaika.
Hakimu Omar Mcha Hamza alihamaki baada ya kushuhudia tukio hilo ambapo aliporejeshwa, aliamuru mtuhumiwa huyo kurudishwa rumande.
“Mdhamini amekataa dhamana yake leo, mbele ya mahakama hii na tunamfutia dhamana yake ambayo alitakiwa kuweka ahadi ya maandishi ya shilingi laki moja na mtuhumiwa kima hichohicho,” alisema hakimu.
Kabla ya kurudishwa rumande, mdhamini wa mtuhumiwa huyo ambaye ni baba yake mzazi, Haji Juma aliiomba mahakama kumfutia dhamana juu ya mtuhumiwa huyo na kuiachia mahakama jukumu hilo, ndipo hakimu alipoamuru kumrejesha tena rumande hadi Septemba 23, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa la shambulio la kuumiza mwili kinyume na sheria.
Hati ya mashtaka iliyowasilishwa mahakamani hapo, ilidai kuwa mnamo Mei 8, mwaka huu, kati ya saa 10:20 huko Mabonde ya Mpunga Mbuzini, Wilaya ya Chakechake, Pemba,  alimshambulia kwa kisu na kumkata vidole vya mkono mlalamikaji (jina linahifadhiwa) na kumsababishia maumivu makal


Love to hear what you think!