Friday, May 10, 2013

Mainda:Baada ya Kubadili Dini yeye na Biblia, Biblia na yeye

MSANII wa filamu ambaye alikuwa Muislam na baadaye kuamua kuingia kwenye Ukristo na kuokoka, Ruth Suka ‘Mainda’ sasa anaonekana kupambana vilivyo kuhakikisha anaiboresha imani yake kwa kutembea na Biblia kila anakoenda.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Mainda aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa msanii huyo anaonekana kuwa na uchu wa kuijua vilivyo Biblia

“Kwa kweli sasa hivi Mainda hakaukiwi na Biblia mkononi, yeye na Biblia kila wakati. Kuna wakati hata akiwa lokesheni, akipata muda kidogo anaitoa na kuanza kuipitia. Hakika amebadilika,” kilisema chanzo hicho huku maneno hayo yakishibishwa na picha alizotupia Mainda kwenye mtandao wake wa Facebook zikimuonesha akiwa ameshikilia kitabu hicho kitakatifu.


Love to hear what you think!