Friday, May 10, 2013

Hatimaye Mume wa Jack Patrick Atoka Jela.


MUME wa mwanamitindo maarufu hapa Bongo, Jacqueline Patrick, Abdullatif Fundikira ‘Tiff”, aliyekuwa jela ya Gereza la Keko jijini Dar alikokuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kufanya biashara ya madawa ya kulevya, amerudi uraiani baada ya kupata dhamana.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Tiff aliachiwa kwa dhamana Ijumaa iliyopita katika Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kusota ‘lupango’ kwa takriban mwaka mmoja.
“Ni kweli sasa hivi Tiff yuko mtaani, ametoka kwa dhamana ila kuhusiana na suala la ndoa yake amesema haipo tena, anaangalia maisha yake,” kilidai chanzo.
Katika kupata ukweli wa habari hii, mwandishi wetu alimpigia simu Abdullatif lakini hakupokea ila Jack alipopatikana alikiri zilipendwa wake huyo kuachiwa kwa dhamana.


Love to hear what you think!