Thursday, April 25, 2013

Nakaya "Moja kati vitu ninavyojutia ni kurudisha kadi ya Chadema na kuingia CCM"

Nakaaya leo hii alikuwa kwenye interview ndani ya XXL, katika mengi aliyoyaongea, moja ni kuhusu kurudisha kadi ya Chadema na kuhamia CCM.

"moja kati vitu  ninavyojutia ni kurudisha kadi ya Chadema na kuingia CCM, najua nimebugi, lakini sio kama watu wanavyoongea kuwa nilipewa hela, kama nilipewa hela si saa hii ningekuwa nakula bata, lakini wapi! mi sijapewa hela.wanajuaje je kama nilitishiwa au vitu vingine kama hivyo..najua hapo nilibugi.Niliingia kwenye siasa kwasababu ya ushawishi wa watu, na nilishawishika kwasababu ya wimbo nilioutoa wakati hui "Mr Politician" lakini baada ya kuingia, niliona kabisa this is not what i can do, siasa ni mchezo mchafu na niliona vinani confuse" amesema Nakaaya


Love to hear what you think!