Friday, November 30, 2012

RIHANNA NA CHRIS BROWN KTK HEADLINES TENA,

Posted: 1st December 2012 by MillardAyo in News
0
                                                 Chris Brown na Rihanna.
 
Wiki moja baada ya mwimbaji Rihanna kupost kwenye page yake ya mtandao wa Instagram picha ya Chris Brown akiwa kitandani bila shati, time hii Rihanna amezidi kuvipa vyombo vya habari cha kuongea baada ya kupost picha nyingine.

Picha yenyewe ni hiyo hapo juu ambapo sasa inazidi kujulikana kabisa kwamba Rihanna na Chris Brown ambao ni wapenzi wa zamani wamerudiana japo hawajawahi kutamka.

Kwa mujibu wa Necole, baada ya kuiweka hii picha RiRi aliandika “I don’t wanna leave! Killed it tonight baby”

Kwenye moja ya interview zake mwaka huu, Rihanna alisema bado moyo wake unamkubali sana Chris Brown na ni ngumu kumsahau maishani.

Picha hizi za Instagram zimezagaa siku kadhaa tu baada ya Chris Brown kutangaza kwamba ameachana na mpenzi wake ili kurejesha amani manake hakua anapenda akiona urafiki wa Chris na Rihanna unaendelea.

Mmiliki wa Gari Alilopata Nalo Ajali Sharo Milionea Aongea

MMILIKI wa gari ambalo lilikuwa likiendeshwa na msanii maarufu nchini, Hussein Ramadhan ‘Sharo Milionea’ na kupata nalo ajali iliyosababisha kifo chake huko Muheza, Tanga, Mohammed Ismaili maarufu kwa jina la Mudi Suma, ameibuka na kueleza uhusiano wake na marehemu, huku akisema amekubali hasara.


Akizungumza kwa simu kutoka Muheza jana Suma alisema hana mpango wa kudai fidia au kupeleka malalamiko yoyote kwa ndugu wa marehemu kwa kuwa; “Kilichotokea ni kazi ya Mungu.” “Siwezi kudai hata kidogo hivyo ni vitu vya kupita tu. Marehemu alikuwa ni zaidi ya ndugu yangu, gari ni kitu kidogo sana katika uhusiano tuliokuwa nao,” alisema Suma na kuongeza kwamba hata Marehemu Sharo Milionea naye alikuwa amemwachia mali zake kadhaa ikiwamo gari.


“Siyo gari tu alilokuwa ameniachia. Kuna mikataba yake ya kazi, Bajaji yake na funguo za chumbani kwake. Nasubiri kukabidhi vitu hivyo baada ya kukaa na ndugu zake. Vitu viko kwenye mikono salama,” alisema.


Kuhusu gari lake lililopata ajali, Suma alisema lilikuwa na bima ndogo, lakini anapanga kwenda TRA atakaporejea Dar es Salaam kufuatilia baadhi ya mambo.
“Kabla ya kuondoka bima ile kubwa ilikuwa imekwisha kwa hiyo nikaamua kuikatia bima ndogo. Nitakapofika kesho (leo) Dar es Salaam, nategemea kwenda ofisi za bima kuzungumza nao,” alisema Suma.


Alipoulizwa kama kuna mtu mwingine atakayeathirika kutokana na gari hilo kuharibika katika ajali mbali na yeye, alijibu: “Hakuna tofauti na mimi mwenyewe na familia yangu.”


Kabla ya ajali
Suma alieleza kuwa kabla ya kuanza safiri yake, Sharo Milionea alifika nyumbani kwake mchana na kumweleza kuwa afya yake haikuwa nzuri.


“Kabla ya kuondoka aliniambia kuwa hajielewi elewi na kifua kilikuwa kinambana. Nikamshauri asiondoke peke yake, atafute mtu wa kuondoka naye ambaye atamsaidia kuendesha gari njiani,” alisema Suma na kuongeza:


“Tulianza kuwapigia simu jamaa zetu wanne wa kusafiri naye lakini kila tuliyemwambia hakuwa tayari. Ilikuwa ni changamoto mpaka ilipofika saa 10:45 hivi jioni, akaamua kuondoka peke yake. Wakati anatoa gari getini kwangu, nikamwambia, basi jaribu kuwa mwangalifu sana, maana alikuwa kweli anasumbuliwa na kifua. Tukakubaliana kwamba atakaporudi aende hospitali kucheki afya yake.”


Kuhusu uhusiano wake na marehemu, Suma alisema: “Mimi ni mfanyabiashara na yeye alikuwa msanii, lakini ilitokea tukawa marafiki sana mpaka ikafikia wakati nikaona kuwa ni ndugu yangu. Nilimwamini nikamtambua kama sehemu ya familia.”


Alisema marehemu alikuwa akitumia gari hilo kila alipolihitaji na safari ya kwenda nalo Tanga kwa wazazi wake ilikuwa ni ya tatu.“Siyo mara ya kwanza kuitumia gari lile, nilikuwa nimemwamini sana. Safari ya kwanza alichukua na kusafiri nalo mwenyewe, halafu safari ya pili ikafuata na hii ilikuwa safari ya tatu,” alisema Suma.


Eneo la ajali wakimbia makazi
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Songa Kibaoni mahala ambako Sharo Milionea alipatia ajali, wamezikimbia nyumba zao baada ya Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu kutoa siku moja kwa waliopora mali za marehemu huyo kuzisalimisha mara moja

HIVI NDIVYO BLACKBERRY ILIVYOSAIDIA KUWANASA WALIOIBA KWENYE AJALI YA SHARO MILIONEA

SIMU aina ya Blackberry ndio chanzo cha kuwanasa wezi pamoja na baadhi ya vitu vilivyoporwa  katika ajali ya msanii wa filamu na muziki nchini, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ eneo la Songa Kibaoni wilayani Muheza mkoani Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe, mapema leo alithibitisha kupatikana vitu hivyo, baada ya msako mkali uliofanywa na uongozi wa serikali wilayani Muheza wakishirikiana na Jeshi la Polisi.
Saluti5 ilimnukuu kamanda huyo akisema: " Jeshi la Polisi liliweka mtego na kutangaza kuinunua simu ya mkononi ya msanii huyo aina ya ‘blackberry’ ndipo moja kati ya wanaodaiwa vibaka waliohusika kwenye tukio hilo, alipojitokeza na kuipeleka kwa ajili ya kuiuza.
"Wakati walipofika eneo ambalo walikubaliana, walikabidhi simu hiyo kwa ajili ya kuikagua, lakini baadaye wezi hao walishtukia mtego huo na kukimbia huku wakiiacha simu hiyo" alifichua Kamanda huyo.
Alivitaja vitu ambavyo vimesalimishwa kwa jeshi hilo kuwa ni simu ya mkononi aina ya blackberry, betri ya gari, tairi la akiba, radio ya gari, begi ambalo lilikuwa na nguo za marehemu, saa ya mkononi na nguo ambazo alikuwa amevuliwa na vibaka mara baada ya kutokea ajali hiyo.Chanzo:www.saluti5.com

Thursday, November 29, 2012

PICHA ZA MASTAA WALIOMZIKA SHARO MILIONEA



Wema Sepetu (kulia) na Jack wa Chuz wakishiriki mazishi ya marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea'.
Yusuf Mlela (kulia) na Sajuki nao wakishiriki mazishi ya Sharo Milionea wilayani Muheza mkoani Tanga jana.…
Wema Sepetu (kulia) na Jack wa Chuz wakishiriki mazishi ya marehemu Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea'.
Yusuf Mlela (kulia) na Sajuki nao wakishiriki mazishi ya Sharo Milionea wilayani Muheza mkoani Tanga jana.
...Ray Kigosi naye alikuwepo.
Swaiba wa marehemu Sharo Milionea, mzee Majuto akiongea machache wakati wa mazishi hayo.
Msanii H- Baba akishiriki kumzika marehemu Sharo Milionea jana.
Steve Nyerere akitoa machache wakati wa mazishi ya Sharo Milionea jana mkoani Tanga.
Mwana FA, Mtitu na Rich wakifuatilia mazishi ya marehemu Sharo Milionea.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia) akimkabidhi Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba ubani wa Airtel kwa ajili ya msiba wa marehemu Sharo Milionea.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA / GPL, TANGA)


1
.
.
.
.
.
Interview na Shetta.
.
Bonge wa mgahawa wa Facebook Kinondoni ambapo Sharo Milionea alikua mara nyingi anakula hapo jioni.
Interview na Dokii.
.
.
.
.
.
Nape Nnauye wa CCM alikuepo pia na mkuu wa Wilaya ya Muheza.
Muhogo Mchungu akipita na kushangiliwa.
.
.
Jackson Mbando kutoka Airtel ambapo aliniambia Sharo Milionea amefariki miezi nane tu baada ya kupata dili la kuwa balozi wa Airtel.
Msanii Tunda Man kutoka Tiptop Connection pembeni yake ni Tembele.
Mwigizaji JB nae alipata tabu baada ya watu kumshangilia na kutaka apige nao picha.
Millard Ayo kwenye interview na JB.
Wasanii wengine niliwahoji wakiwa kwenye magari kama Jackline Wolper manake wakishuka kwenye gari ni vurugu, watu wanang’ang’ania kupiga picha sio kawaida.
.
                               HK ndio alikua meneja wa Sharo Milionea.
.
Gari la huduma ya kwanza lilikuepo ambapo zaidi ya watu 20 walianguka na kuzimia.
Huyu ni mmoja ya waombolezaji ambao walipatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka.
.
.
Huyu ni diwani wa nyumbani kwa kina Sharo Milionea, yeye ndio alikua mtu wa kwanza kutoa taarifa za kifo kupitia CLOUDS FM.
Hii ndio nyumba ya kina Sharo Milionea.
Alipozikwa Sharo Milionea.


Polisi Afukuzwa Kazi kwa Kumbaka Mtuhumiwa wa Kike

JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma, Wilaya ya Momba, mkoani hapa.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Athuman Diwani, askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la Polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la Polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambacho pia kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
Wakati huohuo, katika kijiji cha Malangali Barabara ya Mbeya-Iringa, Wilaya ya Mbarali gari aina ya Nissan Patrol lilimgonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo chake papo hapo.
Alisema kuwa mwili wa marehemu bado haujafamika na mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Chimala Mission na kwamba juhudi za kuutambua mwili wa marehemu na mahali anapotoka zinaendelea.

MUUMINI WA KIISLAMU (SHOGA) NCHINI UFARANSA AJIANDAA KUANZISHA MSIKITI MAALUMU WA MASHOGA WA DINI IYO

Ludovic Mohammed Zahed





Ni wazi kabisa, hili halitawapa faraja waamini wa Uislamu kote duniani, na kwa jinsi ambavyo tumeona migogoro ya kiimani ikiendelea kuigubika dunia siku za karibuni, hili la sasa huenda likafanya migogoro hii ikawa ndio mwanzo wa vita ya tatu ya dunia. Kama huamini, sikia habari hii
Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia, muumini mmoja wa dini ya kiislamu huko nchini Ufaransa, anajiandaa kuanzisha msikiti ambao utakuwa ni mahususi kwa ajili ya waumini wa dini hiyo walio mashoga.
Ludovic Mohammed Zahed, amejiweka tayari kabisa kwa ajili ya kukabiliana sio tu na changamoto atakazokumbana nazo kwa uamuzi wake huo, bali pia kwa mabaya mengine yoyote yatayojitokeza huku akijua kuwa mambo hayo ambayo anajiandaa kuyakabili, lazima yatamtokea. Zahed, sio tu kwamba ni muumini wa kiislamu, bali pia ni mchambuzi aliyebobea katika imani hiyo na anajiandaa kuanzisha msikiti huo katika mji wa Paris, mwishoni mwa mwezi huu.
Tunahitaji kuwa na sehemu ya usalama kwa ajili ya watu ambao wanajihisi hawako salama na huru sana pindi wanapokuwa katika misikiti ya kawaida. Wapo wanawake hawapendi kuvalia vitambaa hadi usoni au kukaa nyuma wawapo misikitini, wapo wanaume ambao hawana hisia za kiume na wanajihisi wanapokuwa mbele za watu hawajisikii uzuri, na mradi huu sasa ni kwa ajili ya kuwaletea matumaini mapya katika kuabudu.

Jackline Afunguka"Nikiachika Tena Naenda Kuolewa Uarabuni"



PAMOJA na kukataa kumwanika hadharani mpenzi wake mpya, staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amesema kuwa akipigwa chini na jamaa yake huyo, atatimka nchi na kwenda kuolewa uarabuni.

Wolper amesema anajitahidi kulilinda penzi lake jipya ili lisiweze kuvunjika na ikitokea hivyo, hatataka  tena kuwa na mpenzi wa  Kibongo.

“Kwa kweli siwezi kuachika tena sasa hivi! Ikitokea sitakuwa na amani moyoni mwangu na sitataka kuwa na mpenzi mwingine hapa nchini, nitaenda kuolewa nje ya nchi,” alisema Wolper ambaye hivi karibuni alimwagana na aliyekuwa mpenzi wake, Abubakar Mtoro ‘Dalas

Wednesday, November 28, 2012

Zamaradi Mketema Afiwa Na Mama YAke Mzazi.


Mtanagazaji maarufu hapa town anaetangaza kipindi cha Take One kina cho rushwa na Televisheni marufu hapa town ijulikanayo kwa jina la Clouds Tv mwanadada Zamaradi Mketema ameripot kuwa amefiwa na Mama yake Mzazi leo asubuhi.
Sababu ya Kifo cha marehemu mama yake Zamaradi ni kwamba alikuwa akisumbuliwa na kansa kwa kipindi kirefu kidogo sasa. Habari hizo tumezipata kutokea kwa mtangazaji mwenzie Zamaradi anaetantangaza kipindi cha ‘Leo Tena’ mwanadada Dina Marrious wa Clouds FM, amesema kuwa alipigiwa simu na zamaradi leo asubuhi huku akiwa na huzuni akimawambia kuwa leo hata weza kufika  kwenye kipindi cha ‘Leo Tena’ kwasababu mama yake amefariki dunia asubuhi ya leo.
Uongozi wa Samatym unaendelea kufanya jitihada ya kumtafuta Zamaradi mwenyewe kwa taarifa kamili zaidi za msiba ulipo na mazishi yatafanyika siku gani. Tunatoa salamu za pole kwa Ndugu,Jamaa na marafiki wa Familia Ya Zamaradi Mketema.