Wednesday, November 28, 2012

Zamaradi Mketema Afiwa Na Mama YAke Mzazi.


Mtanagazaji maarufu hapa town anaetangaza kipindi cha Take One kina cho rushwa na Televisheni marufu hapa town ijulikanayo kwa jina la Clouds Tv mwanadada Zamaradi Mketema ameripot kuwa amefiwa na Mama yake Mzazi leo asubuhi.
Sababu ya Kifo cha marehemu mama yake Zamaradi ni kwamba alikuwa akisumbuliwa na kansa kwa kipindi kirefu kidogo sasa. Habari hizo tumezipata kutokea kwa mtangazaji mwenzie Zamaradi anaetantangaza kipindi cha ‘Leo Tena’ mwanadada Dina Marrious wa Clouds FM, amesema kuwa alipigiwa simu na zamaradi leo asubuhi huku akiwa na huzuni akimawambia kuwa leo hata weza kufika  kwenye kipindi cha ‘Leo Tena’ kwasababu mama yake amefariki dunia asubuhi ya leo.
Uongozi wa Samatym unaendelea kufanya jitihada ya kumtafuta Zamaradi mwenyewe kwa taarifa kamili zaidi za msiba ulipo na mazishi yatafanyika siku gani. Tunatoa salamu za pole kwa Ndugu,Jamaa na marafiki wa Familia Ya Zamaradi Mketema.



Love to hear what you think!