Thursday, July 12, 2012

UMESIKIA KUHUSU KOLABO YA JOSE CHAMELEONE NA SEAN KINGSTON? UNAJUA ANAMLIPA KIASI GANI?Jose Chamelione alipokua Hollywood Marekani pembeni ya sanamu ya Michael Jackson.
Naomba kusema kwamba AY atakua msanii mwenye bahati sana, na hili nalisema kutokana na stori mpya nilizopata kutoka kwenye kinywa cha Jose Chameleone wa Uganda.
Najua unajua kwamba SEAN KINGSTON alipokuja Tanzania alisema anatambua kazi za AY ambapo siku chache baadae AY alitangaza kwamba KINGSTON amekubali kufanya nae kolabo bila kumtoza pesa yoyote, kolabo ambayo ipo hata demo yake nilipewa nikaisikiliza japo bado single haijatoka mpaka sasa.
Tuje kwenye kilichonifanya niandike hayo yote hapo juu, stori ni kwamba Staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone anafanya kolabo na Sean Kingston lakini analazimika kumlipa.

.
Exclusive na millardayo.com Chameleone amesema “narekodi album yangu mpya ambayo ina single kama Valu Valu inaitwa Extra Chameleone, meneja wangu wa Canada ameshaongea na uongozi wa Sean Kingston na amekubali kufanya kolabo lakini bado haijapatikana time ya kufanya video.. mimi kuimba na Sean Kingston na hatujafanya video haita saidia chochote, na kwa kolabo hiyo ya audio na video ninalazimika kumlipa dola za kimarekani elfu 30 ambazo ni zaidi ya milioni 45 za kitanzania”
Kwa kauli hiyo Jose Chameleone amethibitisha kwamba SEAN KINGSTON ndio atakua msanii wa kwanza kumlipa kwa ajili tu ya kufanya nae kolabo ndio maana nilisema ni bahati kwa Ay ambae amepewa nafasi ya bure kufanya kolabo na Kingston, na kilichomfanya pia apate shavu la kufanya kolabo na Romeo Miller na Lamyia ilikua ni baada ya kina Romeo kusikia demo ya kolabo ya Kingston na Ay kwenye studio huko Marekani, ndio wakavutiwa kupiga nae kolabo pia.
Umeonaje hii story, kama umeipenda like au tweet na rafiki zako waione pia.Love to hear what you think!