Baada ya taarifa kuenea kuhusu
uwepo wa msanii Dogo Janja nchini Afrika Kusini kwa show alizopata
zilizofanyika ndani ya wiki tatu, Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo
Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo wake pamoja na matokeo
aliyopata ya kidato cha pili. Michael Alfred Mbaula ambae ni
Afisa taaluma amesema “mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri
na alikua anashirikiana vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara
yake ya mwisho kuingia darasani ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika
kurudia kidato cha pili kwa sababu amefeli kwa wastani mdogo ambao
usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
Kuhusu kauli ya Dogo Janja
kwamba juzi alipokwenda Afrika Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki
mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli kwamba aliomba ruhusa na wala
ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo akitoa taarifa hata katikati
ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za mziki kwa sababu Makongo
ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au mbili ambazo alikua
akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila kukaa miezi
mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
Katika sentensi nyingine,
Mbaula anasema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa kupata wastani wa
27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata sifuri, Civics
alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza 42,
Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”
source . millardayo.com