Msanii
wa kwanza kufanya album hapa Bongo na kwa sasa ni mbunge wa Mbeya mjini
kupitia tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II na wengi
hupenda kumuita Sugu ameonyesha wazi kukerwa na ambao ameuimba ROMA katika ngoma yake ya 2030, Sugu alichodai ROMA ana kurupuka na hajui anachokifanya.
Akizungumza katika kipindi cha TV wiki iliyopita Sugu amesema kuwa
msanii huyo anapaswa kuijua misingi ya hip hop na pia Sugu amemuonya na
kumtaka roma awe muangalifu na anachokiandika na kukitowa kwa jamii
na sio kukurupuka kama mtu aliyestuliwa toka usingizini.
Sugu amesema yeye ni mfuasi wa hip hop hivyo ukitaka kuwa mwana hip
hop lazima uzame ndani sana ili ukiandika kitu uwe na uhakika nacho na
si kufanya kama Roma anavyofanya.Namtahadharisha bwana mdogo awe
muangalifu na anachokiandika na si kukurupuka hip hop ina misingi yake
na ni lazima uzame ndani sana maana hip hop ni maisha na ukweli mtupu,
pia aelewe hip hop ni sauti ya kumkombowa mnyonge sasa unapoimba mambo
ambayo huna uhakika nayo haipendezi maana utakuwa hujaisaidia jamii
husika alisema sugu.
Katika
wimbo huo wa 2030 kuna kipande kina sema pesa ndio imemaliza vita
yaRuge na Sugu kitu ambacho kimeonyesha kumkera Sugu na kusema kuwaRoma
anakurupuka na kuandika asichokijua maana kwa mstari huo tu umefanya
niaamini kila achoandika hana anachokijua maana mstari huu unanihusu na
hakuna ukweli juu ya alichokiimba.
Sugu amemtaka Roma kusikiliza nyimbo walizoimba kaka zake ili zimuongoze katika sanaa yake amesema asikize nyimbo kama za profesa jay,afande sele,solo thang atagunduwa kuwa zilikuwa ni harakati za uhakika mfano mdogo amesema asikilize miss Tanzania ya Solo Thang atajua anachomaanisha.
Roma alipotafutwa kujua amejisikiaje baada ya mheshimiwa kuchukizwa na wimbo wake Roma alisema Sugu ni kaka yake na anaamini kama kuna baya atamuita na atamrekebisha.