Ijumaa ya last week 28th Sept ilikuwa ni birthday ya Wema Sepetu, hakuna asiyemfahamu kutokana na kuandikwa kila kukicha katika magazeti na blogs au webs kutokana na mambo mbali mbali yakiwemo ya mahusiano aliyokuwa nayo na star mwenzake Diamond Platnums na mengineyo.
Katika siku yake ya kuzaliwa hiyo Ijumaa ilisemekana Wema ame ametimiza miaka 22..kwa maana kwamba alizaliwa 28th Sept, 1990. Sawa hilo hata sisi kwetu lisingekuwa na tatizo kabisa sababu huwezi uka judge age ya mtu kama ni kutoka kwake mwenyewe.
Lakini utata katika hili swala ukaanza kujileta kutokana na records ambazo tayari zipo na zinazofanya issue hii iwe na mkanganyiko.
Issue kubwa ni kwamba Wema tayari yupo katika orodha ya walimbwende walioisha wahi kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss World kutokana na yeye kufanikiwa kulinyakua taji la Miss Tanzania mwaka 2006.
Sasa kama alishinda taji la miss Tanzania mwaka huo 2006 takriban miaka 6 kutoka leo, JE, hiyo inamaanisha mwaka huo alioshinda taji hilo alikuwa ana miaka 16?? Kama ndio, hili linawezekana vipi binti aliye chini ya miaka 18 kuruhusiwa kushiriki mashindano hayo?
Na mbaya zaidi akashinda taji na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia
Kama vile haitoshi mapema mwaka huu Wema alifanyiwa Interview na Salama Jabir katika show inayozidi kupata umaarufu kwa sasa ya MKASI.
Moja ya maswali aliyoulizwa Wema ni kuhusu lini alianza kujihusisha na mambo ya mapenzi, na jibu lake lilikuwa alipofikisha miaka 18.
Salama alionesha kutaka kujua zaidi na akamuuliza tena ni lini alifikisha miaka 18, mrembo wema alisita kidogo na kumwonesha Salama kama anaogopa kusema bt end of da day akasema ni kama miaka 5 iliyopita, jibu lililomshtua Salama kidogo lakini akalipotezea na kuendelea na mengine.
Hiyo ni Interview ya mwaka huu 2012, na kama alidai kaanza mahusiano miaka 5 iliyopita that means kwa mujibu wa jibu la wema basi alitimiza miaka 18 mwaka 2007, ambayo bado inathibitisha alishiriki mashindando ya Miss Tanzania 2006 akiwa under 18. Je, aliudanganya umma ili aweze kuruhusiwa kushiriki? .
Mpaka tunakwenda mitamboni jitihada za kumpata Mr Hashim Lundenga wa Lino Agency ambao ndio wandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania kutaka kujua mwaka 2006 ilikuwaje Wema akashiriki katika shindano na kushinda taji hilo ilihali alikuwa under 18 (kama ni kweli), zimegonga mwamba kutokana na simu yake kutopokelewa kwa takribani masaa mawili