SIKU chache baada ya kutangaza kummwaga aliyekuwa mpenzi wake
Ramadhani Mtoro ‘Dallas’, muigizaji Jacqueline Wolper amemfanyia umafia
mchumba wake huyo wa zamani kwa kuliuza gari aina ya BMW X6 lenye namba
za usajili T 574 BXF analodaiwa kuhongwa naye.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii juzikati, mtoa habari wetu ambaye yuko ndani ya TRA inayolishikilia gari hilo kufuatia utata wa ununuzi wake alisema, licha ya kuwa gari hilo liko mikononi mwao lakini si mali ya Wolper tena kwani tayari ameshamalizana na kigogo mmoja anayeshughulikia kulikomboa.
“Kiukweli
kwa sasa hatudili tena na Wolper kwani ameshakuja hapa na mtu ambaye
amemtambulisha kuwa amemuuzia, kwa hiyo masuala yote atakuwa
akishughulikia mteja wake huyo na si yeye,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzipata habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Wolper ambapo alikiri kuliuza gari hilo na kueleza kuwa, kwa sasa anamiliki gari aina ya Toyota IST wakati akijipanga upya.
“Ni kweli sina yoyote kwa sasa zaidi ya hii niliyoinunua hivi majuzi tu na kama umesikia kuwa hata ile BMW nimeiuza, huyo aliyekwambia hajakosea,” alisema Wolper