JAMALI Malinzi amechaguliwa kuwa Rais Mpya wa TFF baada ya kumpiku mpinzani wake Athuman Nyamlani katika uchaguzi mkuu uliofanyika leo na kumalizika usiku huu. Uchaguzi huo, uliotawaliwa na kashkashi za hapa na pale, ulifanyika katika ukumbi wa NSSF WATER FRONT, Dar es Salaam.