Hatimaye
ile ziara ya Muziki Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imeanza
rasmi leo kwa show baab kubwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Katika onyesho hilo lililohusisha wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012
kwa utangulizi wa waendeshaji wake Dulla na Zembwela kutoka East Africa
TV kugawa zawadi kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa kuendesha
mashindano mbali mbali.
Hakuna ubishi kuwa Ben Pol ndiye mfalme wa R&B na alilithibitisha hilo alipoponda jukwaani na kuwaimbisha…
Hatimaye
ile ziara ya Muziki Tanzania iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu imeanza
rasmi leo kwa show baab kubwa katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Katika onyesho hilo lililohusisha wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012
kwa utangulizi wa waendeshaji wake Dulla na Zembwela kutoka East Africa
TV kugawa zawadi kwa mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwa kuendesha
mashindano mbali mbali.
Hakuna
ubishi kuwa Ben Pol ndiye mfalme wa R&B na alilithibitisha hilo
alipoponda jukwaani na kuwaimbisha mashabiki wake mwanzo hadi mwisho kwa
nyimbo zake kali Pete, Jikubali, Samboira huku kivutio kikiwa pale
uwanja mzima ulipoimba pamoja nae wimbo wa Nikikupata.
Malkia
wa Bongo Flava, Lady Jaydee ambaye ni mwanamke pekee katika wasanii
waliokuja Dodoma alithibitisha kwamba habahatishi baada ya kulishambulia
jukwaa kwa nyimbo zake zote zililizompa umaarufu. Jide nae kama wasanii
wengine alianza kwa kumkumbuka marehemu Albert Mangwea kwa kuimba
chorus ya wimbo wa "Sikiliza" ambao ni ushirikiano wake, MwanaFalsafa na
Mangwair kisha kuanza kuimba nyimbo zake kali na kumalizia na Joto
Hasira alioshirikiana na Profesa Jay aliepanda jukwaani kuungana nae.
Profesa
Jay anapenda kuitwa The Heavy Weight MC na alililithibitisha hilo
wakati alipokabidhiwa jukumu la kufunga show, kwa zaidi ya nusu "Jay wa
Mitulinga" kama anavyojulikana aliwaimbisha mashabiki nyimbo zake kali
toka Bongo Dar es Salaam, Chemsha Bongo, Piga Makofi nk. Kivutio
kilikuwa pale alipoimba wimbo wake wa zari la mentali na kumpandisha
jukwaani moja ya mashabiki kuimba mistari ya "Zubeda" huku akishangiliwa
na wengi kabla ya kuendelea kuchana nyimbo zake nyingine zilizompatia
umaarufu.
Alipotajwa
kuwa zamu yake imefika ulitokea mtafaruku wa mashabiki kusukumana kila
mmoja akitaka kuwa mbele ili amuone vizuri, lakini huyu ndiye Mfalme wa
Hip Hop kwa mwaka 2012, Kala Jeremiah ambaye alilishambulia jukwaa kwa
zaidi ya nusu saa huku akwadatisha maelfu waliojitokeza huku kama
kawaida wimbo wake wa Dear God ukionekana kumgusa kila mtu.
Wa
kwanza kupanda kwenye steji alikuwa Linex "Mjeda" alieimba nyimbo zake
zilizotamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni. Wimbo
ulioonekana kuwakonga wengi ulikuwa "Aifola".
Wa
pili jukwaani alikuwa ni Ommy Dimpoz aliepanda jukwaani na madansa wake
wanaosifika kwa uhodari wao wa kumiliki jukwaa na kuimba nyimbo zake
mbili za Baadae na Me and You kabla ya kushuka na kumpisha Ben Pol.
Roma!
Roma! Roma! ndio kelele zilizopigwa na mashabiki wakati akipanda
jukwaani na kama ilivyo kawaida ilikuwa ni michano mwanzo hadi mwisho.
Roma ambaye mwaka jana alishinda tuzo mbili alizidi kuonyesha ubora wake
pale alipoimba nyimbo zake kama "Pastor", "Tanzania", "Kidole cha
mwisho juu" na "2030" huku akitumia dakika kadhaa kumkumbuka marehemu
Albert Mangwair.
---
Show hiyo iliisha mnamo saa
nne huku ikiwa imekidhi kiu ya mashabiki wengi wa burudani wa Mkoa wa
Dodoma na inatarajia kuendelea mkoani Tanga Jumamosi wiki Ijayo.