Monday, May 20, 2013

KILICHOMPATA MADAM RITA KINASIKITISHA!

Na Imelda Mtema
KILICHOMPATA Madam Rita kinasikitisha! Ndivyo unavyoweza kusema ukibahatika kumuona the big boss wa Benchmark Production inayoratibu Shindano la Bongo Star Search, Rita Poulsen ‘Madam’ anayetembelea magongo baada ya kupata ajali mbaya ya gari.
Rita Poulsen ‘Madam’.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda baada ya kuwa kimya muda mrefu ikielezwa kuwa alipata ajali hiyo kitambo, Madam Rita alisema kuwa kwanza kabisa anamshukuru Mungu kwani anaamini kila kitu kinachotokea chini ya jua kina sababu yake na hata alipopata ajali hiyo alimshukuru kwa kutoka salama.
Madam Rita aliendelea kueleza kuwa ajali hiyo aliipata katikati ya Jiji la Dar  na kusababisha kuvunjika kwa kifundo ‘enka’ cha mguu wa kulia hivyo kumsababishia kutembelea magongo baada ya hospitali kumuwekea ‘hogo’.

“Namshukuru Mungu kwanza kwa kunitoa salama katika ile ajali japokuwa sijapona vizuri,” alisema Madam Rita.
Mkurugenzi huyo aliendelea kueleza kuwa alipopata ajali hiyo alikimbizwa katika Hospitali ya Muhimbili kwenye Taasisi ya Mifupa ya Moi lakini hali ilipokuwa kuwa mbaya alihamia katika hospitali moja ya Kichina ambapo kwa sasa amepata nafuu.

Sunday, May 19, 2013

MMILIKI WA JAMIIFORUMS NA NDUGU ZAKE WAPATA AJALI MBAYA


Mmoja wa waanzilishi na wamiliki wa Jamii Forums, Maxence Melo, amepata ajali ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza; kilometa chache kutoka Nzega mjini. 
Mwanzilishi mwenzie na msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema Maxence na ndugu yake ambaye naye alikuwepo kwenye ajali hiyo, walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi. 
Bw. Mushi amesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana. Haijaelezwa Bw. Maxence melo ameumia kiasi gani, ila taarifa zinasema kuwa ndugu yake amejeruhiwa vibaya .
Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali
Waanzilishi/wamiliki wa JamiiForums, Mike Mushi(kushoto) na Maxence Melo(mwenye koti) aliyepata ajali

VUGURU ZATOKEA MJINI IRINGA, POLISI WATUMIA MABOMU KUREJESHA AMANI

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa baada ya Machinga kufunga barabara kuu ya Iringa - Dodoma na ile ya Mashine Tatu mjini Iringa leo.
Hali ikiwa tete eneo hilo.
Polisi wakiwa tayari kukabiliana na Machinga.
 Abiria na wapiga debe wa stendi kuu Iringa wakinawa maji baada ya  kupigwa mabomu na kumwagiwa maji ya kuwasha na askari.
(PICHA ZOTE NA FRANCIS GODWIN, IRING

Saturday, May 18, 2013

Baada ya Kuhamia Kenya Yasemekana Mr Nice Arudia Maisha ya Matanuzi na Mademu

Old habits die hard and for the case of Tanzania’s artist Mr. Nice, it seems like he has gone back to his old ways. Well, word had it that he had gone broke after he spent away all his money in parties and women. (Mac Muga)

According to sources, Nice who is currently planning to shoot a video for his latest track Chali wa Kibera has been seen club hopping with a number of Kenyan women.

He is painting tables red in hang out joints for his women who seem to have a soft spot for him. A fan who is worried alleges that he may just drift away again to poverty if he continues with his behavior.

Source:The Kenyan Daily Post

MTOTO ALIYEPIGWA MAPANGA NA BABA YAKE AFARIKI DUNIA


Mtoto Devotha Gerald (4) aliyepigwa mapanga na baba yake, polisi mstaafu Samson Bwire Amefariki dunia baada ya jitihada za madaktari kuokoa maisha yake kushindikana...
 
Mtuhumiwa wa tendo hilo ambaye naye alipigwa vibaya na wananchi wenye hasira yuko mikononi mwa jeshi la polisi....
 
Tendo hili lilitokea mkoani Shinyanga. 
Kama haukuona habari hiyo ya kusikitisha, ya kushambuliwa mtoto huyo, iliyotokea juzi usiku, nenda kwenye link ifuatayo: Polisi mstaafu amcharanga mapanga mwanae wa miaka 4

UNYAMA: POLISI AMCHARANGA MAPANGA MWANAE WA MIAKA 4 KISA KIKIWA NI WIVU WA MAPENZI


MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI KWA HUDUMA AYA KWANZA.
WANANCHI WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.
KINA MAMA WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI
HAPA AFANDE AKIWA HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..
MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
MADAKTARI WAKIWA KAZINI KUHAKIKISHA WANAOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PINGU.
JITIHADA ZA KUOKOA MAISHA YA MTOTO ZIKIENDELEA
INASIKITISHA SANA JAMANI
MAJUKUMU YA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO YAKISONGA KWA KASI.
AFANDE BWIRE AKIWA NA PINGU ZAKE WODINI
MUNGU AMPE AHUENI MTOTO HUYU.


KAHAMA 

Mkazi wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), ameshikiliwa na jeshi la polisi kwa kumcharanga mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi....


Tukio hilo limetokea jana jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani.....


Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akichoma nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata mapanga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.

Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani.......


Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumuua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.

Hata hivyo Wakati gari la Poisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.

Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.na mwanaafrika