Tuesday, June 2, 2015

Mambo 9 Aliyoyasema Fredrick Sumaye LEO Wakati Akitangaza nia yake ya Kuwania Urais Kupitia CCM


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe. Fredrick Sumaye ametangaza nia ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro jijini Dar leo.
 
Sumaye amesema kuwa ameamua kutangaza nia akiwa Dar es Salaam maana anataka kuwatumikia Watanzania wote siyo wa nyumbani kwake pekee.
 
Kauli mbiu yake ni ‘Uongozi Bora, Komesha Rushwa, Jenga Uchumi’.

Haya  ni  Baadhi  ya  Mambo  aliyoyasema;

1.Anaongelea mafanikio katika katika kipindi yuko madarakani ikiwemo televisheni ya taifa, uboreshaji elimu ya msingi. Anasema leo badala ya sekondari nayo kupanda ndio hio imeshuka.
 

2.Anaongelea sera ya ubinafsishaji, anasema sera hio ilikuwepo kabla ya uongozi wa Mkapa. Hivyo wao walikuwa watekelezaji na hawawezi kulaumiwa. Ubinafsishaji kama sera ni kitu muhimu na ni vizuri ilifanyika. Mashirika zaidi ya asilimia 45 yamenunuliwa na watanzania, mengine kwa ubia na wageni na asilimia ishirini pekee yalinunuliwa na wageni kwa asilimia 100.
 

3.Nimekumbana na mambo magumu katika miaka hio kumi ikiwemo ajali ya MV Bukoba na ajali ya treni, ukame wa mwaka 1997. Niliunda kamati ya kushughulikia jambo hilo na kuchimba visima zaidi ya 300 Dar es Salaam. Mambo magumu yalinikomaza katika uongozi. Mvua za El nino zilifata baada ya ukame, ilikuwa hali ya hatari lakini tulijikwamua na tuliendelea na kazi wa kujenga taifa letu. Kifo cha baba wa taifa, mimi sikulala siku tatu nzima hata kwa nusu saa, sijawahi kuona kipindi cha amani kama kili, polisi waliripoti hata uhalifu haukuwepo.
 

4.Wakati waziri mkuu, sikuweza kusikia watu wanapigana, asubuhi nisiwepo pale, leo wakulima na wafugaji wanapigana miezi sita sasa. Mfano mgogoro wa waancholi na wahadzabe.
 

5.Huwezi kuzungumzia amani wakati watu wana njaa, tatizo la uchumi, watu wanaangalia takwimu badala ya uhalisia. Tunatakiwa tuendeleze kilimo, hata wakati wa Nyerere tulileta matrekta lakini tuliendelea? Kuleta matrekta ni jambo jema sasa nitalima heka 50, lakini uwezo wa mbegu heka 3 na kupalilia heka 3.
 

6.Eneo lingine muhimu ni masoko, lazima kiendelezwe katika ukubwa wake. Wakulima watauza kwa bei ya hasara na bei ikiwa vizuri hawana tena mazao. Leo viwanda vya sukari, hatuwezi kuingiza sukari kutoka nje bila kodi, lazima tulinde viwanda vyetu vya ndani. Mazao yetu yote, kama tutakua na juhudi za kusindika mazao, hili tatizo la ajira ambalo tunapiga nalo kelele sana, litapungua. Pia pengo kati ya walionacho na wasio nacho litapungua.
 

7.Nimeona shule binafsi wanafanya vizuri, wanataka wazipunguze nguvu, ongeza juhudi nawe umfikie. Katika miaka miwili au mitatu tutapunguza kwa kiasi kikubwa wanaoenda nje.
 

8.Rushwa na ufisadi, hili jambo sina utani nalo. Ukituhumiwa kwa rushwa ndani ya wiki moja unachunguzwa na wiki mbili mahakama imekuhukumu na kama ni viboko unapokea kabisa.
 

9.Nawashukuru ndugu zangu waandishi wa habari, nimezungumzia Dar es Salaam na naamini mtafikisha nchi nzima ili tumpokee rais Kikwete kijiti ambae amefanya vizuri. Kama kuna maswali pia niko tayari


Love to hear what you think!