Saturday, December 20, 2014

MZAZI MWENZIYE SUGU AVAA PAMPASI UKUMBINI

Stori: Imelda Mtema
Kituko! Katika hali ya kushangaza, msanii wa filamu Faiza Ally ambaye amezaa na Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, aligeuka kituko baada ya kuingia ukumbini akiwa amevalia mavazi wavaayo watoto kuhifadhi haja zao maarufu kama ‘pempasi’.
Faiza akiwa na pempasi ukumbini.
Tukio hilo lilitokea juzikati katika Hotel ya Sea Cliff iliyopo Masaki jijini Dar, ambako walialikwa watu wachache kwa ajili ya kula chakula cha jioni pamoja.
Wakati wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini huku wakifikiria jinsi mwenyeji wao atakavyotinga hotelini hapo, ghafla walimuona Faiza akiingia ukumbini akiwa ndani ya mavazi hayo yaliyosindikizwa na kishati kidogo alichovaa juu na kuwafanya waalikwa wote kuangua kicheko.
...Akiwa na rafiki yaake.
“Nimefikiria sana kwa nini nianze kujipa gharama za nguo na nilipomuangalia mwanangu Sasha anavaaga pempasi na mimi nikasema ngoja nifanye hivyo,” alisema Faiza.
Faiza akiwa na Sugu.
Faiza na Sugu waliodumu katika uhusiano kwa miaka mingi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja, Septemba, mwaka huu walimwagana na sasa kila mmoja amechukua hamsini zake.

Love to hear what you think!