Monday, January 28, 2013

TASWIRA KATIKA PICHA ZA HALI ILIVYOKUWA WAKATI WA VURUGU MKOANI MTWARA

 

Moja ya nyumba ikiteketea wakati wa vurugu mkoani Mtwara ambapo magari 18, pikipiki 7 viliteketezwa kwa moto  vyote vikiwa ni mali za halmashauri ya Masasi na baadhi ni vya watumishi wa halmashauri hiyo.
Gari la wagonjwa likiteketea kwa moto.
Sehemu ya magari yakiendelea kuteketea kwa moto.
Jengo la Mahakama lililochomwa moto.
Chumba cha Jenereta kilichochomwa moto.
Nyumba inayosemekani ni nyumba ya waziri ikiwa imeharibiwa vibaya.
Nyumba inayosemekana ni ya Mwenyekiti wa CCM baada ya kuharibiwa.
Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa vurugu hizo.

Thursday, January 24, 2013

AIBU YA MKE WA MTU


Issa Mnally na Richard Bukos
KITUKO cha aina yake kimejiri Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Meeda Sinza jijini Dar wakati Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo’ ilipokuwa ikitumbuiza, Amani linakumegea kilichotokea.

Katika onesho hilo, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu alifanya kitendo cha aibu baada ya kusaula nguo zake zote na kubakia na nguo za ndani.
Katika onesho hilo, Extra Bongo ilikuwa ikiwashindanisha mashabiki wake kucheza staili yao ya Kizigo na washindi kujinyakulia zawadi za fedha.
Wakati bendi hiyo inayoongozwa na ‘Kamarade’ Ally Choki ikitoa burudani, ghafla mwanamke huyo (jina lake halikupatikana) alivamia jukwaa na kuanza kucheza kwa staili aliyokuwa akiijua mwenyewe.

Mpigapicha wetu alipojaribu kumpiga picha dada huyo alihamaki na kumjia juu huku kumtishia kumvunjia kamera yake huku akidai kuwa yeye ni mke wa mtu, hivyo hapaswi kupigwa picha.
“Mimi ni mke wa mtu ukifanya mchezo nitakutolea laana,” alisema mwanamke huyo huku akizishika nguo zake na kuanza kuzitoa mwilini mwake  moja baada ya nyingine.
Wakati mwanamke huyo akiendelea na zoezi lake la kusaula nguo, alijitokeza dada mwingine ambaye  aliambatana naye pamoja ukumbini hapo na kumwita  kwa jina la wifi.

“Wifiii…, wifiii…, weee wifii pombe gani hizo, usivue nguo, usifanye hivyo ni aibu,  itakuwaje kaka akiziona hizo picha magazetini?” alisema dada huyo aliyedaiwa kuwa ni wifi mtu lakini pamoja na kumpigia kelele hizo haikusaidia kumzuia  mwanamke huyo mcharuko kusaula nguo zake.
Baada ya kuombwa sana na wifi yake, mwanamke huyo alivaa nguo zake na kuendelea na burudani hadi mwisho.
Haikufahamika mara moja kama mwanamke huyo alifanya  kitendo hicho kutokana na pombe au hasira za kupigwa picha.

Wednesday, January 23, 2013

RAIS KIKWETE AMALIZA ZIARA YAKE YA UFARANSA LEO



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Orly, Ufaransa, baada ya kumaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tano nchini humo leo Januari 23, 2013.
(PICHA NA IKULU

FLAVIANA MATATA ATWAA TUZO YA MWANAMITINDO BORA WA AFRIKA 2012



photo

Tuzo aliyojishindia mwanamitindo Flaviana Matata.



---

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameendelea kung’ara kimataifa baaada ya kushinda tuzo ya Nigeria’s Next Super Model na kuwa mwanamitindo bora barani Afrika wa mwaka 2012 (Africa’s Most Outstanding Model 2012).


Tuzo hiyo utolewa kwa wanamitindo ambao bado wanailetea sifa Afrika kimataifa na Flaviana amekuwa katika chati ya juu. Mwaka jana Desemba,  Flaviana alishinda tuzo nyingine  ya uwanamintindo bora kutoka kwa diaspora ya Waafrika.


Flaviana ambaye kwa sasa  anaishi na kufanya kazi ya uanamitindo New York nchini Marekani kupitia shirika la Wilhelmina Models, mpaka sasa ameweza kuitangaza Tanzania kimataifa kutokana na umahiri wake katika maonyesho ya mavazi.


Tangu ashinde taji la Miss Universe Tanzania mwaka 2007, Flaviana amekuwa aking’ara katika kona zote za dunia na hasa baada ya kumaliza katika nafasi ya sita katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, huku Tanzania ikishiriki kwa mara ya kwanza.


Ameweza kushiriki katika maonyesho ya mavazi mengi Ulaya na Amerika huku akitoa misaada mingi kwa Watanzania wenzake ambao wamekuwa na ndoto ya kufika mbali katika fani hiyo.


Kwa sasa Flaviana anaendesha taasisi yake, Flaviana Matata Foundation ambayo inasomesha watoto wa kike 16 na mwaka jana alitoa msaada wa vifaa vya kuokoa maisha kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba huku ikiwa kumbukumbu ya kifo cha mama yake mzazi katika ajali hiyo ya mwaka 1996.


Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Compass Communication Tanzania Limited, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa wamejisikia faraja sana kwa kumvumbua mwanamitindo huyo ambaye kwa sasa anashika chati ya juu Tanzania na nje ya nchi.


Maria alisema kuwa Flaviana amedhihirisha ubora wake na mpaka sasa amepitiliza kiwango cha kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake, ndoto ambayo alikuwa nayo muda mrefu.

Tuesday, January 22, 2013

"NIMENUNUA GARI MPYA......MNAONICHUKIA KAZI MNAYO"...WEMA SEPETU


Wema sepetu
Picha za Gari mpya  ya  Wema Sepetu aina ya Audi Q7 yenye rangi nyeusi zimeonekana kwenye akaunti ya Wema ya Instagram alipokuwa beach hivi karibuni na kuiandikia caption, ‘my baby at da beach.’
gari wema
Kwenye akaunti ya meneja wake Martin Kadinda pia kuna picha nyingine ya gari hiyo aliyoiandikia maneno, ‘#maisha sio manhattan…..You can creat your own Manhattan in Tz… Hata kama ni Ya muda mfupi… #Kiphating.’
gari wema 2
Gharama ya gari hiyo inaweza kuanzia shilingi milioni 70 na kuendelea.

MWANACHUO WA SAINT JOHN, DODOMA AUAWA KIKATILI


JESHI la polisi mkoani Dodoma limeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa kinyama kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima na watu wasiojulikana.

Marehemu Lidya mwenye umri wa miaka 57 anadaiwa kuuawa siku ya jumapili hii majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa maeneo ya chuo hicho chenye wanafunzi 5500
akiwa anarejea nyumbani baada ya masomo ya jioni.

Ni simanzi,vilio,huzuni na majonzi katika vyunga vya chuo hiki kufuatia tukio hili la kusikitisha ambalo linadaiwa kuyaweka katika mashaka na wasiwasi mkubwa maisha ya wanafunzi hawa.


Licha ya kulitupia lawama jeshi la polisi baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa baada ya kufikwa na mkasa huo uliositisha safari ya maisha yake mwili wa marehemu Lidya uliharibiwa vibaya na mnyama asiyejulikana kwa kunyofolewa macho,masikio,pua,mguu na viuno vingine.


Prof.Gabriel Mwaluko ni makamu mkuu wa Chuo na Karimu Meshack ni afisa habari ambao kwa pamoja wanaelezea kilichorjiri.


Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo, Kamanda wa mkoa ACP David Misime anawataka wakazi wa mkoa huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.


Wakati huo huo Kamanda Misime anasema msako mkali umeanza wa kuwatia nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwa ajili ya hukumu.

Sunday, January 20, 2013

SAKATA LA GESI: MTWARA NI MABOMU NA RISASI ZA MTOTO



MABOMU na risasi za moto jana zilitawala katika mji wa Mtwara na vitongoji vyake baada ya wananchi kufanya maandamano makubwa kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam.

Maandamano hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Bara, Julius Mtatiro, ambaye alifuatana na wabunge wa chama hicho wanaotoka mikoa ya kusini.

Maandamano hayo yamefanyika baada ya maandamano mengine makubwa yaliyofanyika Desemba 27 mwaka jana kwa lengo hilohilo, yakiwa yamendaliwa na vyama vinane vya siasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, maandamano ya jana yalifanyika huku wanawake wakiwa mstari wa mbele.
Chanzo cha kupigwa mabomu hayo kinaelezwa kuwa ni kukatika kwa umeme katika eneo ulikokuwa unafanyika mkutano wa hadhara wa CUF ambako wananchi waliahamaki na kuandamana kwenda ofisi za Tanesco Mtwara i kujua chanzo kukatika kwake.

Wakiwa njiani kuelekea Tanesco umati huo mkubwa wa wafuasi wa CUF ulikutana na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ambao waliamua kuwatawanya kwa mabomu na kupiga risasi za moto hewani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mtatiro jana, lengo la kufanya maandamano na mkutano huo lilikuwa ni kupokea karatasi ya kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam
Alisema akiwa katika mkutano huo alipokea saini 10,000 za wananchi wa mikoa ya kusini ambao wanapinga mpango huo wa serikali kuisafirisha gesi. 

Maandamano hayo yalihitimishwa na mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara na wabunge wa CUF waliokuwapo ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Magdalena Sakaya (Tabora), Mbunge wa Mkanyageni Habib Mnyaa, Salum Barwan (Lindi Mjini), Said Bungara "Bwege" Kilwa Kusini na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mtwara, Clara Mwituka.

Mtatiro alisema msingi wa hoja yao ni kujikita katika kuhakikisha gesi inatumika kwa faida ya taifa lakini kwa kutoa kipaumbele katika maeneo yaliyo nyuma katika maendeleo, kama kusini.

Watu wakamatwa mitaani
Kutokana na vurugu hizo inaelezwa kuwa zaidi ya watu 20 walitiwa mbaroni na jeshi la polisi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mary Nzuki hakuweza kupatikana jana kwa simu yake ya kiganjani. 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mtwara, Tutufye Mwakagamba alikiri kukamatwa kwa watu kadhaa katika vurugu hizo ingawa alimtaka mwandishi wa habari hizi amtafute baadaye.

“Ni kweli ndugu yangu kuna watu kadhaa tumewakamata katika vurugu zilizotokea leo (jana), lakini ninakuomba nitafute baadaye kwa sababu muda huu nipo katika mkutano wa CUF ambako kuna mvua kubwa inanyesha,” alisema Kamanda Mwakagamba.

Biashara zafungwa
Kutokana na maandamano hayo yaliyoambatana na vurugu biashara mbalimbali zilifungwa katika soko kuu la Mtwara na mitaani hali iliyowafanya wananchi kuwa katika wakati mgumu.

Magari ya CUF kila kona
Habari zinasema mkutano wa jana ulikuwa na shamrashara za aina yake na zaidi ya magari 14 yalisafirisha wafuasi wa CUF kutoka wilayani Tandahimba wakati magari mengine manane yalitokea wilayani Newala.

Wakati huohuo, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (CCM), ameibuka na kuitaka serikali kutodharau madai ya wananchi wa mikoa ya kusini kuhusu suala la gesi.

Aliyasema hayo wiki chache baada ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kufanya maandamano ya amani kupinga ujenzi wa bomba la kusarisha gesi kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.

Dk. Ndugulile, alisema kwa mtazamo wake suala hilo lina sura mbili tofauti ambayo yote yana hoja za msingi ikiwamo umaskini wa mikoa ya kusini na tataizo la ajira kwa vijana

Saturday, January 19, 2013

MWANDISHI WA GAZETI LA MWANAHALISI, SAED KUBENEA AJIPANGA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CHADEMA

Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi Saed Kubenea, inasemekana amejapanga kugombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kupitia CHADEMA mwaka 2015. kwa hivi sasa Jimbo hilo linaongozwa na Silvestry Koka [CCM].

Hii itakuwa habari njema kwa tasnia ya habari kujiingiza katika masuala ya uongozi wa kisiasa, Kubenea kapata msukumo wa kugombea Ubunge baada ya kushauriana na Dr Slaa na kumuakikishia kuwa anaweza kushinda Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini kama akijipanga vizuri na kupata msaada wa CHADEMA.

Kila la Heri Saed Kubenea

WAKE ZA WATU 13, WANAFUNZI 18, MAHOUSE GIRL 7 NA MABAAMEDI 5 WANASWA WAKIJIUZA


HAIWEZI kuwa aibu mpaka siri ifichuke, kwa wake za watu 13 walionaswa wakijiuiza, kwao imekuwa zaidi ya kuumbuka, wametia fedheha ndani ya familia zao.

Wake hao za watu, walinaswa usiku wa Jumanne iliyopita, Barabara ya Shekilango, kuanzia Afrika Sana mpaka Mori, Sinza, Dar es Salaam, wakati jeshi la polisi lilipofanya msako maalum wa kushtukiza.
 Pamoja na wake hao za watu, vilevile wanafunzi 18 wa vyuo mbalimbali nchini, mahausigeli saba na mabaamedi watano, arobaini yao ilifika siku hiyo, walipokamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Mabatini kabla ya kupandishwa kizimbani, Mahakama ya Jiji siku iliyofuata.

Katika msako huo, zaidi ya makahaba 60 walikamatwa na katika mahojiano na polisi, ikabainika kuwapo kwa wake hao za watu, wanafunzi, wahudumu wa baa na wafanyakazi wa ndani.

WAKE ZA WATU.......
Jeshi la polisi likichukua maelezo ya mmoja baada ya mwingine, askari mmoja alimfikia mwanamke aliyefahamika kwa jina la Suzan Moses ambaye katikati ya mahojiano, alijieleza kwamba ni mke wa mtu.

Suzan ambaye baadaye ilibainika kwamba hujulikana pia kwa jina la Mamaa Suzy, alijieleza kuwa anaishi na mume wake  Tandale, Dar es Salaam na wana watoto wawili.

Askari aliyekuwa anamhoji Suzan, aliuliza: “Mke wa mtu kweli na watoto wawili unajiuza, huoni kama ni hatari?”

Suzan: “Hatari naijua ndiyo maana simruhusu mwanaume yeyote aniingilie bila kondomu, nipo makini juu ya hilo.”

Askari: “Mumeo anajua kama unajiuza?”

Suzan: “Hajui, japokuwa hata yeye tulikutana viwanja. 

Nilimdanganya mimi ni mhudumu wa Corner Bar, akaniachisha kazi lakini baada ya kuona hanitimizii mahitaji muhimu, nikamwambia narudi kazini, kwa hiyo mpaka leo anajua nahudumia baa.”

Baada ya wote kuhojiwa, ikabainika kuwa katika wanawake hao 60 waliokamatwa, mbali na Suzy, walikuwepo wengine 12 ambao ni wake za watu.

Mwanamke mwingine, Jessica Mashaka alidai kuwa aliamua kujiuza baada ya kubaini kwamba mume wake analelewa na mwanamke mmoja tajiri jijini Dar es Salaam.

“Anachokifanya mume wangu ni sawa na mtu anayejiuza. Akipewa fedha na mwanamke wake ananinyanyasa ndani ya nyumba, nikaona na mimi nijiuze nipate fedha zangu mwenyewe ili aache kuninyanyasa.”
 
Hata hivyo, Leila Madaha alidai yeye na mume wake walikubaliana ajiuze ili wawe wanapata fedha za kujikimu.

 Alisema: “Mume wangu huwa ananisisitiza kutumia kondomu kwa kila mteja, yeye hana kazi tangu alipofukuzwa bandarini miaka minne iliyopita.”
 WANAFUNZI......
Wanafunzi 18 kutoka vyuo vya Dar es Salaam, Dodoma na Iringa, walijitambulisha katika mahojiano na hayo na polisi.

Wanafunzi wa mikoani walisema kuwa hali ni mbaya kibiashara huko tangu iingie Januari ndiyo maana wamekuja Dar kujaribu kutafuta kipato.

MABAAMEDI NA MAHAUSIGELI.......
Katika wanawake hao, ilibainika wapo mabaamedi watano ambao walidai kuwa vipato vyao ni vidogo ndiyo maana kila baa wanazofanyia kazi zinapofungwa saa 5:00 usiku, hulazimika kuingia mitaani kuuza miili waweze kupata fedha zaidi za kuwawezesha kuishi.


Vilevile, wapo mahausigeli saba ambao maelezo yao yalikuwa sawa na yale ya mabaamedi kwamba hulipwa ujira mdogo na mabosi wao ndiyo maana hulazimika kujiuza ili kuongeza vipato.

Thursday, January 17, 2013

"RAY HAIJUI HATA NGUO YANGU YA NDANI....NAOMBA NIWEKE WAZI KUWA SI MPENZI WANGU"...SAJENT


BAADA ya ishu kuvuja kuwa msanii wa filamu Husna Idd ‘Sajenti’, ana mahusiano ya kimapenzi na ’Ray’, amezikana habari hizo huku akisisitiza kuwa msanii huyo anamchukulia kama kaka yake na suala la kutoka naye kimapenzi halina ukweli wowote.

Tukio la Sajenti kutoka na Ray lilianza kuskika pindi kundi la bongo movie lilipoenda mkoani Mwanza kucheza mchezo wa kirafiki na wasanii wa mkoani humo.


Mtandao huo ulitaka kujua Sajenti anazungumziaje habari hizo, ambapo alidai kuwa hajawahi kutoka na  ’Ray’  kimapenzi na anayesambaza ishu hizo ana nia ya kumchafua ingawa alishindwa kueleza anachafuliwa kwa namna gani.


Alisema kuwa kama zingekuwa na ukweli taarifa hizo angeweka wazi lakini haoni sababu ya kukubali wakati kitu hajawahi kukifanya na wala hana wazo wa kutoka na msanii huyo kwani mpenzi wake anamtosha.


“Sijawahi kutoka kimapenzi na  Ray na  hajui  hata  nguo yangu ya  ndani na kama una ukweli kama unajua natoka naye kwanini umepiga simu na kuniuliza,??.. nasema sijawahi kutoka naye,” alidai.

Hata hivyo msanii huyo aliongeza kuwa kama mwanaume aliwahi kutoka naye hawezi kuficha lakini juu ya Ray atakanusha siku zote.

Wednesday, January 16, 2013

MTOTO MCHANGA AKUTWA AMETUPWA KANDO YA MTO KARIBU NA CHUO KIKUU CHA TUMAINI

Mtoto wa jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa ametelekezwa pembeni ya mto karibu na chuo kikuu cha Tumaini Iringa.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama zaidi  katika eneo hilo na hii inaonesha jinsi gani watu wasivyo na utu.


"Inavyoonekana mtu huyu alijifungua halafu akamtupa mtoto huyu, hii ni ajabu sana kwa mtu kubeba mimba miezi tisa halafu kuamua kutupa kiumbe kisicho na hatia" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja Rajabu

Kwa mujibu wa kijana aliyeona mwili huo alisema alikuwa anaelekea shambani na ndipo alipoamua kupitia sehemu ambayo huwa anaficha jembe na kuona kiumbe huyo akiwa ametelekezwa huku akiwa amekwisha kufa.

"Inawezekana mtu huyu alimtupa mtoto huyu usiku kwani jana wakati naficha jembe hapakuwa na kitu chochote "alisema kijana huyo.

HOUSE GIRL AJINYONGA MAENEO YA TABATA SHUHUDIA HAPA

Dada wa kazi za nyumbani wa eneo la Tabata Barakuda aliyejiua jana saa moja usiku na bado chanzo hakijulikani
Machela ya kubebea mwili wa marehemui ilifika
Waliuingiza mwili wa mdada huyu mwenzetu na kuondoka nae ambapo blog hii itaendelea kuwajulia taarifa kuhusiana na kile kilichomsibu mdada huyu
Watu wakiuchungulia mwili wa marehemu
Umati wa watu ulikusanyika kujua nini chanzo
Inasemekana kuwa hilo ni tukio la pili kujitokeza katika eneo hilo
Hapa kazi yao ikiendelea ya kuhoji wahusika
Maaskari Polis wa kituo cha Rozana wakichukua maelezo

MAPAJA YA SINTAH YAANIKWA HADHARANI


Tumezoea kushuhudia  vituko  vya  Wema  Sepetu, Rayuu, Wolper  na  Wengine......Sasa  hali imebadilika.

Msanii  wa kibongo  kwa  maana  halisini kioo  cha jamii ambaye  mara  nyingi huwa mstari wa  mbele kuikemea jamii na kuionya pia.....Maonyo  hayo huifikia jamii kupitia kazi zao  za sanaa.....


Wasanii na  Waalimu  ni mfano  hai wa kuigwa  kimaadili  hasa  katika kipindi hiki kigumu cha UTANDAWAZI. 

Jamii itawashangaa kama mtafkia hatua  ya kuukumbatia "UZUNGU"  na  kuukana "UAFRIKA"

  HIZI NDO COMMENT  ZA  WADAU  BAADA YA KUYAWEKA  HAYO MAPAJA YAKE  HADHARANI KUPITIA BLOG YAKE.....
 

"SERIKALI HAITAVUMILIA TENA VURUGU ZOZOTE ZA KIDINI, KIKANDA AU KIKABILA:"...RAIS KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete
SERIKALI imesema haitavumilia kwa namna yeyote ile vurugu za kidini, kikanda na ukabila ambazo baadhi yake zilitaka kulitia doa taifa mwaka jana.

Pia imesisitiza kwamba haitawavumilia wanasiasa wanaotumia rasilimali za taifa kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuligawa taifa.

Akizungumza na mabalozi kwa nyakati tofauti Ikulu, Dar es Salaam; kwanza katika sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya iliyofanyika juzi na alipokuwa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini, Dianne Corner jana, Rais Jakaya Kikwete alisema vurugu zilizotaka kujitokeza mwaka jana zinatosha.

“Serikali haitavumilia vurugu wala ukabila kwa namna yoyote ile…. Mwaka 2012 vurugu zenye sura ya kidini zilianza kujitokeza ila sasa nasema kwamba hatutazivumilia kwa namna yeyote ile, inatosha,” alisema Rais Kikwete.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kiongozi wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Mpango alisema jumuiya ya mabalozi imefurahishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa ikishughulikia vurugu za kidini ambazo zilitaka kujitokeza bila kusababisha madhara kwa wananchi.

“Tumeridhishwa na namna ambavyo Serikali imekuwa inashughulikia mambo yake vizuri. Tunaomba mwendelee kushughulikia amani ya nchi hii maana ndiyo mhimili wa nchi za Maziwa Makuu,” alisema Balozi Mpango