Thursday, December 5, 2013

AJIUA BAADA YA KUMTUMIA MUMEWE MESEJI YA MPENZI WAKE

Marehemu Gail Crocker wakati wa uhai wake.
POLISI mwanamke nchini Uingereza, PC Gail Crocker (46), alijiua siku za karibuni baada ya kuandika ujumbe mfupi wa simu (meseji) kwa mpenzi wake akimshukuru kwa “burudani” waliyofaidi walipokutana kwa siri – lakini, kwa bahati mbaya, aliituma meseji hiyo kwa mumewe.
Katika meseji hiyo, Crocker aliandika kwamba: “Ningependa tuwe tunafanya hivi kila mara.” Tukio la  wawili hao lilitokea wakati mumewe Crocker akiwa safarini kibiashara.
Uchunguzi uliofuatia tukio hilo la kujiua kwa Crocker ulibaini kwamba baada ya mumewe kurejea nyumbani huko St Stephen, Cornwall, ulizuka ugomvi na mwanamke huyo mwenye watoto wawili alikunywa vidonge vingi na kufariki.
Na mumewe, Peter Crocker (49) alisema: “Gail alikuwa ndiyo maisha yangu.”
Chanzo: METRO
Love to hear what you think!