ZIARA YA RAIS KIKWETE MAKETE MKOA WA NJOMBE
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia ubora wa shati lililotengenezwa na
wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha wilaya ya Makete baada
ya kukifungua rasmi chuo hicho mwishoni mwa juma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA cha wilaya ya Makete mwishoni mwa juma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiongea na Bi Sarah
Mageni Sanga, mlemavu ambaye Rais alimpa pikipiki ya Bajaj pamoja na
mtaji wa pesa taslimu wa shilingi milioni mbili Oktoba 28, 2009 baada ya
kuguswa na mkasa wa maisha ya mkazi huyo wa kijiji cha Lupalilo wilaya
ya Makete mkoa wa Njombe alipomuona akihojiwa katika TV na kueleza kuwa
maisha yake ni magumu mno baada ya ndugu na jamaa zake wote kuteketea
kwa maradhi ikiwa ni pamoja na UKIMWI. Pichani Bi Sanga akimshukuru Rais
kwa msaada huo ambao amesema umebadili kabisa maisha yake kwani sasa
anaishi kama mtu yeyote kijijini hapo.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongeana wananchi wa kijiji cha Ivalalila
wilayani Makete baada ya kuweka jiwe la msingi la kituo cha afya cha
kijiji hicho mwishoni mwa juma.
Rais Kikwete akitoka kuweka jiwe la msingi madarasa ya kidato cha tano Shule ya Sekondari Lupalilo