Sunday, October 13, 2013

Taarifa kuhusu mwandishi wa ITV Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi


                                         Rais Jakaya Kikwete akiwa na Ufoo Saro
Mwandishi wa ITV Ufoo Saro amejeruhiwa kwa risasi iliyopigwa na mwanaume mmoja alieripotiwa kutokua na maelewano mazuri ambapo kwenye hili tukio mwanaume huyu alimpiga risasi na kumuua mama mzazi wa Ufoo Saro.
Mwanaume huyu alimpiga Ufoo risasi mbili ambazo zilimjeruhi na kudhani kwamba amemuua na kisha yeye mwenyewe kujipiga risasi na kufariki.
Mambo yote haya yalitokea huko Kibamba ambapo taarifa zisiso rasmi zinasema kwamba huyo mwanaume baada ya kuwa na ugomvi kati yake na Ufoo, alienda kuongea na mama mzazi wa Ufoo baada ya kuona mama yupo upande wa Ufoo ndio akaamua kuua.
ITVLove to hear what you think!