Sunday, September 22, 2013

UPDATES SHAMBULIO LA KIGAIDI NCHINI KENYA: 59 WAMEUAWA, 175 WAKIJERUHIWA

Baadhi ya…
Baadhi ya majeruhi wakitolewa eneo la shambulio na wengine kupatiwa huduma ya kwanza.
Taarifa kutoka serikali ya Kenya ni kwamba mpaka sasa watu 59 wameripotiwa kuuawa na 175 wakijeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate lililopo jijini Nairobi, nchini Kenya.
Taarifa hiyo imetolewa kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya Kitaifa, Joseph Ole Lenku.
Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo lililovamiwa ni kati ya 10 na 15.
Shirika la Msalaba Mwekundu awali katika taarifa yake lilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika shambulio hilo.
Mpaka sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi pamoja na vifaru vikiwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ya mateka.
Rais Uhuru Kenyatta katika taarifa yake amesema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake na miongoni mwa waliofariki ni mwanadiplomasia wa Canada na raia wawili wa Ufaransa.
(PICHA ZOTE KWA HISANI YA AP/GETTY IMAGES NA REUTERS

Love to hear what you think!