Saturday, July 20, 2013

ROSE NDAUKA ANA MIMBA?

Stori:Hamida Hassan
MSANII wa filamu Bongo, Rose Ndauka huenda akawa ana mimba kwani hivi karibuni aliugua ghafla alipokuwa ‘lokesheni’, presha ikampanda pamoja na kichefuchefu.

Tukio hilo lilitokea maeneo ya Tegeta ambapo msanii huyo akiwa katikati ya ‘kushuti’ filamu ya Jawabu, alianza kujisikia vibaya na kuomba apewe msaada.

“Hatukujua kilichompata, ghafla alituambia anajisikia vibaya,” alisema mtoa habari.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Rose kupitia simu yake ya mkononi ambapo alikiri kusikia kichefuchefu na kusema hakujua kilichompata lakini alipewa dawa za kutuliza maumivu na sasa anaendelea vizuri na kuahidi kwenda kupima mimba.Love to hear what you think!