Saturday, June 8, 2013

Kitimtim cha Kili Music Awards 2013 leo!

 

Hatimaye siku imetimia, ile siku ambayo kila mja na muungwana katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya alikuwa akiingoja, usiku wa tunzo za Kilimanjaro Tanzania, zitaunguruma kuanzia saa moja hadi kuendelea, Watanzania takriban 32 wanaofanya kazi katika tasnia ya muziki wanatarajiwa kuondoka na tunzo mikononi mwao leo.
Zaidi ya wasanii 100 wametajwa kuwania tunzo hizi, na wote wana imani ya ushindi na watakuwa ukumbini leo pamoja na baadhi ya mashabiki wao, kushuhudia matokeo ya kazi ngumu waliyoifanya katika msimu uliopita wa muziki wa Tanzania.
Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro, kilichodhamiria kupeleka muziki wa Tanzania katika kilele cha mafanikio, leo ndiyo mwenyeji wa shughuli husika na wameahidi usiku wa kihistoria, huku wakiadhimisha mwaka wa 13, wa tunzo hizi ambazo kila kukicha zinazidi kujizolea umaarufu.
George Kavishe, ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro na amefanya mahojiano na gazeti hili kuhusiana na usiku wa leo na mambo muhimu makubwa matatu yametajwa katika kuunogesha usiku mwingine wa tunzo, uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu.
Kwanza, usiku hautakuwa Dar es Salaam peke yake utakuwa katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro na Dar ambapo katika viwanja mbalimbali vya Taifa Dar es Salaam, Mabatini Mwanza, na CCM Mkoa kwa Kilimanjaro kutakuwa na TV kubwa zitakazokuwa zikionyesha moja kwa moja tukio la utoaji tunzo litakalokuwa likiendelea katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa leo.
Watazamaji wa mikoani, watashuhudia tunzo hizo kwa kiingilio cha bia moja tu milangoni, na wakiingia katika viwanja hivyo watakuta maandalizi mazuri kutoka kampuni ya bia Tanzania, na watakuwa wakishuhudia onesho lote, pamoja na burudani mbalimbali zitakazokuwa zinatolewa na waandaaji.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam watakaopata bahati ya kuhudhuria onesho hilo ambapo kiingilio kitakuwa Sh 75,000 kwa watu maalumu na kawaida itakuwa Sh20,000.
“Sababu mbili za msingi za kuweka onesho hili uwanjani, kwanza, ni kutokana ma mfumo wa digitali, ambapo Watanzania wengi wameshindwa kukabiliana nao kutokana na hali ya kiuchumi, hivyo tumewapa fursa nyingine ya kushuhudia tunzo, lakini pia tungependa mashabiki wakae pamoja na kushuhudia tukio hili la kihistoria,” alisisitiza George Kavishe.
Red Carpert
Hili ni zoezi litakalohusisha mastaa hasa upande wa mitindo, ambapo picha zitakuwa zikichukuliwa, katika kuperuzi nani kaja vipi na kavaa nini na alikuwa amesindikizwa na nani.
Hii itakuwa na mtangazaji wake na itakuwa ni kama sehemu ya kipindi cha TV na kwa habari tulizonazo, ni kwamba mtangazaji wa Channel O na mdau mkubwa wa burudani, Jokate Mwegelo ndiye atakuwa mwendeshaji.
Kwa mujibu wa waandaaji, zoezi litachukua kama saa limoja hivi, maana shughuli yenyewe itaanza saa mbili usiku


Love to hear what you think!